Home LOCAL UTENDAJI WA MADAWATI YA KIJINSIA WAENDELEA KUIMARIKA – DKT. GWAJIMA

UTENDAJI WA MADAWATI YA KIJINSIA WAENDELEA KUIMARIKA – DKT. GWAJIMA


Na: WAMJW-MOROGORO

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima ameweka wazi kuwa Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeendelea kuimarisha utendaji wa Madawati ya Polisi ya Jinsia ili kuongeza kasi ya kushughulikia changamoto za ukatili wa kijinsia inayoendelea katika jamii yetu.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Desemba 2, 2021 wakati wa hafla fupi ya kufungua kituo cha pamoja cha mkono kwa mkono (one stop center) katika chuo kikuu kishirikishi cha Jordan kilichopo Mkoani Morogoro.

Amesema kuwa, mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia nchini yanaendelea kuimarika ambapo mashauri 20,025 ya ukatili yalishughulikiwa ikilinganishwa na mashauri 18,270 yaliyoripotiwa mwaka 2019/20.

“Katika kipindi cha Julai 2020 – Juni 2021, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeendelea kuboresha utendaji wa Madawati ya Polisi ya Jinsia, huku akiweka wazi kuwa, katika kipindi hiki, Madawati yamepokea na kushughulikia jumla ya mashauri 20,025 ya ukatili ikilinganishwa na mashauri 18,270 yaliyoripotiwa mwaka 2019/20.” Amesema.

Mbali na hayo amesema, Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutoa huduma katika vituo 14 vya mkono kwa mkono nchini katika Hospitali za Serikali za Amana, Mwananyamala, Tumbi, Iringa, Tabora, Sekou Toure, Mbeya FFU, Simiyu, Shinyanga, Kahama, Hai, Kitete, Mount Meru na Nindo.

kusema kuwa , Katika kipindi cha Julai 2020 – Juni 2021, waathirika 1,857 wa ukatili wa kijinsia walipata huduma, kati yao watoto ni 1,072, Wavulana wakiwa 412 na Wasichana wakiwa 660, huku Wanawake wakiwa 785.

“Katika kipindi cha Julai 2020 – Juni 2021, waathirika 1,857 wa ukatili wa kijinsia walipata huduma kati yao watoto 1,072 (Wavulana 412 na Wasichana 660) na Wanawake 785.” Amesema Dkt. Gwajima

Aidha,  Dkt. Gwajima amesema, Katika kipindi cha Julai 2020 – Juni 2021, jumla ya watoto 167 (Wavulana 111 na Wasichana 56) na Wanawake 269 walipata huduma katika nyumba salama 6 zilizoanzishwa katika Mikoa ya Arusha (2), Kigoma (1), Mara (2), Moshi (1).

Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema, Serikali imeendelea kushughulikia mashauri ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo ukatili wa kimwili, kihisia, kingono na kiuchumi.

Nitoe rai kwa viongozi wa Wizara ya Afya na wadau wote wa ulinzi na usalama kwa Mtoto kuendeleza ushirikiano uliopo ili kuhakikisha mradi huu unazaa matunda ya mfano kwa Mkoa na nchi nzima. Amesema.

Mbali na hayo Dkt. Gwajima ametoa rai kwa Wanaume wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia na wake zao katika familia wajitokeze ili Serikali iweze kuwasaidia kupata haki stahiki.

“Tunafahamu wapo wanaume wanaofanyiwa ukatili katika maeneo mbali mbali hususan katika ngazi ya familia zao, naomba nitoe wito kwa wanaume wote wanaofanyiwa ukatili katika maeneo yote mjitokeze, mtoe taarifa ili kuweza kupata haki zenu “Amesema.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martin Shigella amesema kuwa, katika Mkoa wa Morogoro bado hali ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na Wanawake ipo juu, huku akiweka wazi dawa kama Mkoa wamejipanga kukabiliana na changamoto hiyo.

Pia, amemshukuru Waziri wa Afya, Dkt. Gwajima kwa kuendelea kufuatilia kwa ukaribu uboreshaji wa huduma za afya, na kuweka wazi kuwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro utatekeleza maelekezo yote ambayo yatatolewa na Wizara.

Mwisho.

Previous articleRAIS ALHAJ DKT.HUSSEIN MWINYI AONGOZA WANANCHI KATIKA SALA YA JENEZA KUMSALIA MAREHEMU MWANAJUMA MRISHO MASJID MABLUU
Next articleWATAKIWA KUTUMIA KAMPUNI ZILIZOSAJILIWA BRELA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here