Home LOCAL TURKEY YAIMARISHA USAFI ZANZIBAR

TURKEY YAIMARISHA USAFI ZANZIBAR

Muonekano wa gari za kusafirishia taka ngumu kwaaajili ya kuimarisha usafi zilizozinduliwa na Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed huko viwanja vya kumbu kumbu ya mapinduzi Kisonge, chini ya udhamin wa V-CLEAN wakishirikiana na Baraza la mji zanzibar.

Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa  na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed  akikata utepe kuzindua gari za kisasa za kubebea taka ngumu kwaajili ya kuimarisha usafi ,hafla iliyofanyika viwanja vya kumbukumbu za mapinduzi Kisonge.

Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed akizindua mifuko maalum ya kuhifadhia taka laini,taka za matumizi ya majumbani na taaka za mahotelini kwaajili ya kuimarisha usafi, hafla iliyoandaliwa na V-CLEAN wakishirikiana na Baraza la Manispaahuko Viwanja vya kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.

Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed akizindua mifuko maalum ya kuhifadhia taka laini,taka za matumizi ya majumbani na taaka za mahotelini kwaajili ya kuimarisha usafi, hafla iliyoandaliwa na V-CLEAN wakishirikiana na Baraza la Manispaahuko Viwanja vya kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.
 

Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mh.Masoud Ali Mohammed watatu kutoka kulia,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana,mwenyekiti kampuni ya vigor Taufik Turkey wakiwa na viongozi mbalimbali wa manispaaa , wakionyesha mifuko maalum ya kuhifadhia taka laini ,taka za matumizi ya nyumbani,na taka za hotelini ,mara baada ya uzinduzi WA mifuko hiyo huko viwanja vya kumbukumbu za mapinduzi Kisonge Zanzibar.
 
Waziri wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohammed akiwa ndani ya moja ya gari alizozizinduwa kwajili ya kuimarisha usafi kupitia kampuni ya wawekezaji wa V-CLEAN ili kukagua zaidi gari hiyo,hafla iliyofanyika viwanja vya kumbukumbu za mapinduzi Kisonge.


Na: Khadija Khamis -Maelezo 

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mheshimiwa Masoud Ali Mohamed amewataka wananchi kuziunga mkono jitihada za  Serikali katika kuhakikisha mji unakuwa safi.

Kufanya hivyo kutaisaidia Zanzibar kuwa na haiba nzuri ambayo itaweka ustawi bora na kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mifuko maalum ya kuhifadhia taka pamoja na gari za kisasa za kusafirishia zilizotolewa na Kampuni ya Vigor huko katika Uwanja wa Mapinduzi Square Kisonge .

Amesema  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt,Husein Mwinyi ametoa rai yenye dhamira njema kuhakikisha mji unakuwa safi hivyo iko haja ya wananchi kushirikiana kwa pamoja kudumisha usafi katika maeneo yao.

Aidha alisema Kampuni ya Vicline itashirikiana na Serikali  kuondoa changamoto iliyopo ya kusambaa  taka taka katika mji jambo ambalo linapoteza haiba na ustawi wa mji .

Alifahamisha suala la kujenga nchi sio la serikali pekee bali ni jukumu la wananchi wote hivyo iko haja ya mashirikiano ili kuhakikisha azma iliokusudi inafikiwa.

Waziri Masoud alisema licha ya taka kuna uchafuzi wa mazingira ya kubandika  matangazo mengi kiholela bila ya kufuata utaratibu kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa Kitwana Mustafa  alisema bado mji haujaridhisha hasa katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambao ni jicho la Zanzibar hivyo sheria ndogo ndogo zipitiswa kwa kutoa faini kwa wanaochafua mji .

Alisema ni vyema jamii kuimarisha mji kwa kupanda bustani mbali mbali katika maeneo yao ili kuengeza uzuri wa mji wa Zanzibar.

Nae Mkurugenzi wa Manispaa Mjini, Ali Khamis alisema Baraza la Manispaa  kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa taka kumetokana na gharama kubwa ya uendeshaji, uchakavu na uwezo mdogo wa vifaa vya ukusanyaji wa taka pamoja na uchache wa rasilimali watu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kampuni Vigor ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Taufik Salum Turkey amesema kampuni hiyo inamkakati wa kuzisarifu taka kwa lengo la kubuni miradi na kuzalisha viwanda vidogo vidogo vya vyakula vya kuku majongoo mbolea  pamoja na karatasi jambo ambalo litasaidia kutoa fursa nyingi  za ajira kwa vijana.

Akitoa wito kwa jamii alisema usafi ni jukumu la wote hivyo tushirikiane tuimarishe mji kwa pamoja na Kauli Mbio ya Uzinduzi huo ni Weka Mji Safi kwa Utalii bora Zanzibar.

 

Previous articleWAZIRI JAFO ATOA MAAGIZO MAZITO MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI
Next articleWAZIRI MAKAMBA ATAMANI MWELEKEO MPYA REA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here