Home SPORTS TUMEJIPANGA KIVITA NCHINI ZAMBIA: PABLO

TUMEJIPANGA KIVITA NCHINI ZAMBIA: PABLO




Na: Stella Kessy

KOCHA Mkuu wa Simba Pablo Franco amesema wamejipanga kwa mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows utakaopigwa Jumapili nchini Zambia japo utakuwa mgumu.

Pablo amesema anajua  Red Arrows kwa kutaka kupindua matokeo lakini simba wanamtaji wa mabao hivyo wamejipanga kuhakikisha wanalinda ushindi.

Kauli hiyo leo  wakati akiwa uwanja  wa ndege wa Julius Nyerere pamoja na kikosi wakiwa tayari kuelekea zambia kwa ajili ya mchezo huo.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu Red Arrows watataka kishinda lakini tumejipanga kupambana nao, kikubwa tunahitaji kulinda ushindi wetu tuliopata mchezo  uliopita”amesema.

“Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na morali ipo juu na tunafaham kitu gani kinatakiwa kuelekea mchezo wa jumapili ili kuwapa furaha mashabiki wetu”amesema

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here