Home LOCAL TEMDO NDANI YA MIAKA 60 YA UHURU TUMEFANIKIWA KUHAULISHA TEKNOLOJIA KWA JAMII.

TEMDO NDANI YA MIAKA 60 YA UHURU TUMEFANIKIWA KUHAULISHA TEKNOLOJIA KWA JAMII.

Dkt. Sigisbert Mmasi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) akiongea na waandishi wa habari

Dkt. Sigisbert Mmasi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) akielezea teknolojia wanazozitengeneza kwa mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela, spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki Martin Ngoga pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi kutoka wila na halmashauri za mkoa wa Arusha


Baadhi ya wanafunzi mkoani Arusha wakiangali vifaa tiba vinavyotengenezwa na TEMDO

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) ndani ya miaka 60 imefanikuwa kuhaulisha teknolojia mbalimbali wanazozibuni kwa jamii na kuweza kusaidia kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla kutokana na wananchi kujiajiri kupitia teknolojia hizo.

Akiongea na waandishi wa habari katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru yaliyofanyika kimkoa Dkt. Sigisbert Mmasi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko alisema kuwa wameweza kusanifu mitambo mbalimbali ikiwemo ya kusaga na kukoboa kwa kuwapa michoro wajasiriamali watengenezaji ili waweze kutengeneza kibiashara lengo likiwa ni TEMDO kujiwekeza zaidi kwenye utafifi na sio kufanya biashara.

Alisema kuwa tokea TEMDO ilivyoanzishwa mwaka 1980  hadi sasa imeweza kutengeneza mashine zaidi ya 60 lakini pia ina viwanda vilivyokamilika  6 ambazo ni kiwanda cha kutengeneza unga wa lishe, siagi ya karanga, teknolojia ya kutengeneza nishati mbadala pamoja na  kiwanda Cha kutengeneza viungo.

Dkt Mmasi alifafanua kuwa pamoja na hayo pia wamefanikiwa kutengeneza mashine za kukamulia mafuta ya alizeti, mashine za kusindika juisi za aina mbalimbali, mashine ya kutengeneza siagi inayotoka kwenye maziwa ya Ng’ombe, mtambo wa kukamua mafuta yatokanayo na michikichi, mashine ya kusindika asali, mashine ya kupukuchua mahindi pamoja na mashine kuteketeza taka za hosipitali na taka ngumu.

Alieleza kuwa pia wamefanikiwa kutengeneza vifaa tiba vya aina 16 ambapo baadhi ni kitanda kwaajili ya kujifungulia, kitanda ambacho Daktari anatumia kumkagua mgonjwa, kitanda cha kumlaza mgonjwa, loka za kuhifadhia vitu vya mgonjwa  pamoja na kifaa vya kutundikia dripu.

“Kwahiyo utaona kuwa TEMDO  ni taasisi ya kihuandisi inayojaribu kugusa kila sekta kwani tunatoa huduma zitazoweza kusaidia katika sekta tofauti tofauti ikiwemo pia huduma za viwandani kama kuistol kiwanda, kuhamisha, kufundisha mainjinia na mateknishan pamoja na mambo mengine mengi kwahiyo nawakaribisha wale wote wanaotaka kuwekeza waje TEMDO ili kuweza kupata maelekezo sahihi na mashine bora zitakazofanya wafanye uwekezaji wenye tija,” Alisema Dkt Mmasi.

Alisema kuwa pia wamefanikiwa kutengeneza mashine ya kutenganisha nyanya na megu zake baada ya wazo hilo kupelekwa kwao na kampuni mojawapo ya mbegu hapa nchini ambao walikuwa wanapata changamoto kutenganisha mbegu na nyanya kwa hekari nyingi ambapo mashine hiyo waitengeneza waliweza kuuza mpaka South Afrika.

“TEMDO tunauwezo wa kutoa suluhu pale mteja anapokuwa na tatizo la kiteknolojia lakini pia kwa kuzingatia kuwa uchumi wa nchi inategemea zaidi kilimo teknolojia nyingi zinalenga katika usindikaji na kuongeza thamani mazao ya kilimo ili kukuza uchumi wa taifa kwa kuongeza thamani ya bidhaa na ufanisi wa kazi,” Alisema.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Arusha John Mongela wakati alipotembelea banda la tasisi hiyo katika maonesho yaliyoenda sambamba na maadhisho ya miaka 60 ya Uhuru alisema kuwa  ni vema tasisi ikaendelea kutengeneza mitambo yenye ubora lakini pia itayotatua changamoto za kiteknolojia zilizopo hapa nchini kwa sekta zote kwani jambo wanalolifanya ni zuri pamoja na kuwataka kujitangaza zaidi ili kuweza kuwafikia wananchi wa maeneo yote ya nchi ya Tanzania pamoja na nchi za nje.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here