Na: Hughes Dugilo: ZANZIBA.
katika kuelekea katika kilele cha sherehe za miaka 60 wa Uhuru wa Tanganyika Shirika la Uakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeendelea kutoa elimu kwa umma ili watanzania waweze kufahamu shughuli mbaimbali na majukumu yanayotekelezwa na shirika lao.
Akizungumza na wadau pamoja na wananchi mbalimbli waliotembelea kwenye Banda lao katika Maonesho ya Sekta ya Viwanda yanayoendelea katika viwanja vya Maisala Mjini Zanzibar Afisa Uhusiano Mwandamizi Amina Miruko amesema kuwa yapo majumu ambayo wanayasimamia na kuyafanya kwa mujibu wa Sheria ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi katika nyanja mbalimbali ususani masuala ya usalama wa abilia anapokuwa kwenye usafiri wa maji.
Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimmizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.
Aidha Shirika hilo pia lina wajibu wa kuhimiza ufanisi, uchumi na uaminifu, kuendeleza upanuzi wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji, kuhimiza ushindani katika biashara ya uwakala wa meli, na kuingia kwenye majukumu ya kimkataba na watu wengine au kikundi cha watu.
Akizungumzia Maonesho hayo Amina amesema kuwa yamekuwa na mwamko mkubwa nakwamba kumekuwa na watu wengi wanaopita kwenye Banda lao kwaajili ya kutaka kufahamu majukumu ya Taasisi yao ikizingatiwa imekuwa ni mara ya kwanza kuwepo kwa maonesho hayo Zanziber.
“kuna mwamko wa watu wamekuwa wakipita hapa na kupata elimu ili watambue nini tunafanya lakini pia wao kama wananchi kufahamu majukumu ya Shirika lao, ndio mana tupo hapa ili kutoa fursa kwa wadau wote na wananchi wa Zanzibar kwa ujumla kufahamu shughuli zetu” Amesema Amina.
TASAC wameshiriki katika Maonesho hayo ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Zanzibar yenye kaulimbiu isemayo “MIAKA 60 TANZANIA IMARA KAZI INDELEE” yanafikia kilele chake Disemba 9 Mwaka huu yakienda sambamba na Shamrashara za kumbukizi ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo kilele chake ni tarehe 9 Disemba, 2021.