Home SPORTS TANZANIA WAFUZU KOMBE LA DUNIA

TANZANIA WAFUZU KOMBE LA DUNIA
 Na: stella Kessy, DAR ES SALAAM.

WAZIRI wa  Michezo nchini Mhe, Innocent Bashungwa leo  amewapongeza wachezaji wa timu ya Tanzania (Tembo Warriors) kwa  kufuzu  hatua ya nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa   wenye ulemavu (CANAF 2021).

Hata hivyo Tanzania imekuwa timu nne kati ya ambazo zitaingia katika michuano ya kombe la dunia huko mwakani.

Tanzania imepata  tiketi ya kushiriki  Mashindano ya Dunia  ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon  mabao 5-0.

Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo  tembo ilishinda  goli 1-0.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara  baada ya mechi hiyo kuisha Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuisaidia  timu  hiyo ili kuendelea na  kufanya vizuri  katika maandalizi ya Kombe  la Dunia.

Amesema  kwa  kuwa  safari ya kuelekea  kombe la  dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa  kombe  linabaki  Tanzania.

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na  Alfan Kyanga dakika ya  2 na 15 , Ramadhan Chomole  dakika ya  18, na Frank Ngailo  dakika ya  36 na  44.

Mchezo huo pia umeshuhudiwa na  Rais wa Mashindano hayo duniani  Mateus Wildack.

Previous articleHABARI ZILIZOPO MAGAZETI YA LEO J.TANO DISEMBA 1-2021
Next articleTEMBO WARRIORS WAIBAMIZA CAMEROON 5-0
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here