Na: stella Kessy, DAR ES SALAAM.
WAZIRI wa Michezo nchini Mhe, Innocent Bashungwa leo amewapongeza wachezaji wa timu ya Tanzania (Tembo Warriors) kwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021).
Hata hivyo Tanzania imekuwa timu nne kati ya ambazo zitaingia katika michuano ya kombe la dunia huko mwakani.
Tanzania imepata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Dunia ya mchezo huo yatakayofanyika nchini Uturuki 2022 baada ya kuichapa timu ya Cameroon mabao 5-0.
Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga timu ya Morocco 2-1 na Sierra Leone ambapo tembo ilishinda goli 1-0.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mechi hiyo kuisha Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili kuendelea na kufanya vizuri katika maandalizi ya Kombe la Dunia.
Amesema kwa kuwa safari ya kuelekea kombe la dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa kombe linabaki Tanzania.
Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na Alfan Kyanga dakika ya 2 na 15 , Ramadhan Chomole dakika ya 18, na Frank Ngailo dakika ya 36 na 44.
Mchezo huo pia umeshuhudiwa na Rais wa Mashindano hayo duniani Mateus Wildack.