Home LOCAL TAMASHA LA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA LA FANA JIJINI DAR, TUZO ZATOLEWA

TAMASHA LA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA LA FANA JIJINI DAR, TUZO ZATOLEWA

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fanti (kulia) akikabidhi Tuzo kwa kwa Pili Maguzo (kushoto) Mkurugenzi wa Bahati Fimale Band kutokana na kazi wanazofanya katika kutunga na kuimba nyimbo za kuielimisha jamii na kupinga ukatili wa Kijinsia.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fanti akizungumza kwenye Tamasha la hisani muda mfupi kabla ya kukabidhi Tuzo.
Mwalimu Joyce Kiyango (kushoto) wa Shule ya Awali ya One Planet iliyopo Dodoma akipokea Tuzo yake aliyoipata kutokana na umahiri wake wa kuwafundisha watoto kwa namna ya kucheza nao muziki na michezo mbalimbali.
Balozi wa Ujerumani nchini Regine Hess akizungumza wakati wa Tamasha hilo kabla ya kukabidhi Tuzo.



Wasanii kutoka katika Bendi za Muziki wa Kitanzania wakitumbuiza kwenye Tamasha hilo.

Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni Ubalozi wa Ufansa Cecile Frobert Akizungumza kwenye Tamasha hilo. (PICHA NA HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fanti  amesema kuwa  ukatili wa Kijinsia hapa nchini unaweza kupungua kwa kiasi kubwa endapo Jamii itashirikiana kwa pamoja kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau mbalimbali wa Maendeleo  katika kupinga na kukomesha vitendo hivyo.

Balozi Fanti ameyasema hayo Disemba 8 Mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa ukatili wa Kijinsia katika jamii sio jambo la kupuuzwa kwani linakandamiza uhuru wa wanawake na wasichana wadogo katika kupata  haki zao.

Amesema kuwa Dunia ipo katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia nakwamba tatizo hilo halipo kwenye Bara la Afrika pekee bali ni swala la kiulimwengu ikiwemo ulaya.

“Mapambano haya sio kwa Bara la Afrika tu, bali Dunia nzima ikiwemo ulaya, wote wanapambana na tatizo hili, hivyo ni lazima tuungane kwa pamoja kuhakikisha ukatili wa kijinsia unapungua kwa kiasi kikubwa”Amesema Balozi Fanti.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Utamaduni Ubalozi wa Ufansa Cecile Frobert amezungumzia Tamasha la hisani la kupinga ukatili wa Kijinsia lililoambatana na utoaji wa Tuzo mbalimbali kwa watu binafsi na Taasisi zilizoshiriki katika kutoa mchango wao kukomesha vitendo vya  ukatili wa Kijinsia hapa nchini ambapo wasanii walioshiriki Tamasha hilo waliimba nyimbo za jamii kupinga ukatili wa kijinsia.

Wasanii walioshiriki katika tamasha hilo ni Siti & the Band, Shikandoto Band, Ben Pol, na Nandi, huku kukiwa na mwitikio mkubwa wa wananchi na wadau mbalimbali waliojitokeza kushiriki kwenye Tamasha hilo.

Katika hatua nyingine Tuzo mbalimbali zilitolewa katika tamasha hilo  kwa wadau na Taasisi zilizoshiriki kuunga mkono juhudi za Serikali na Wadau mbalimbali kupinga ukatili wa Kijinsia hapa nchini ambapo walipata Tuzo hizo.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Magharibi Kati TABORA Dkt. Isaac Kissiri Laiser ambaye ni kati ya waliopata Tuzo hizo, amsema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya utumikishwaji watoto kwenye mashamba ya tumbaku ambapo kumepelekea watoto wengi kutokwenda shule kutokana na ugumu wa maisha katika familia zao.

“Tatizo hili kwa Tabora limekuwa kubwa kwenye baadhi ya wilaya ndio maana nikaamua kuanzisha Programu maalum ya kuziwezesha familia zao kwa kuwapatia mikopo ili kufanya biashara ndogo ndogo zitakazowawezesha kupata mahitaji ya watoto wao” Ameeleza Askofu Laiser.

Wengine ni pamoja na Mwalimu Joyce Kiyango wa Shule ya awali ya One Planet iliyopo Dodoma aliyepata Tuzo kutokana na umahili wake wa kuwafundisha watoto kwa namna ya kucheza nao muziki na michezo mbalimbali ya kitoto na kuwafanya watoto hao kufurahi na kupenda kwenda shuleni.

“Nimejisikia furaha sana kupata Tuzo hii mana hiki ni kitu ambacho nilikua nafanya tu ili watoto wapende masomo lakini sikutegemea kama ingenifanya kufahamika na kufikia hapa leo, kwakweli imenipa faraja sana” Ameongea Joyce huku akiwataka walimu wengne kuwa na ubunifu katika ufundishaji ili watoto waweze kupenda masomo na kuelewa kwa haraka wanachofundishwa.

Katika tukio hilo pia Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania Manifredo Fanti alipata fursa ya kukabidhi Tuzo kwa Pili Maguzo Mkurugenzi wa Bahati Fimale Band kutokana na kazi wanazofanya katika kutunga na kuimba nyimbo za kuielimisha jamii na kupinga ukatili wa Kijinsia, ambapo Mwakilishi kutoka Clouds Media Group alikabidhi Tuzo kwa Flora Lauwo ambaye ni  Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee Foundation ya Jijini Mwanza.

Tamasha hilo la kupinga ukatili wa Kijinsia limefanyiika ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia iliyolenga kuhamasisha kuhusu athari za ukatili, hasa kwa wanawake na wasichana wadogo ambapo kampeni hiyo ilianza rasmi tarehe  Novemba 25, Mawaka huu ikiwa inalenga kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Wasichana wadogo Duniani.

 PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA TAMASHA HILO.







Previous articleRAIS SAMIA- MIAKA 60 YA UHURU,KISWAHILI KIMEKUA KIMATIFA
Next articleTEMDO NDANI YA MIAKA 60 YA UHURU TUMEFANIKIWA KUHAULISHA TEKNOLOJIA KWA JAMII.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here