Home ENTERTAINMENTS TAIFA CUP 2021 MUSIC CHALLENGE YAMALIZIKA KWA MIKOA KUTOA MASTAA WAPYA

TAIFA CUP 2021 MUSIC CHALLENGE YAMALIZIKA KWA MIKOA KUTOA MASTAA WAPYA


Na Mwandishi Wetu
 

“Ngoja niseme hili najua wapo ambao hawatanielewa, kwa jinsi unavyoimba na kukaa kwenye key hakuna msanii yeyote katika ‘top five’ ya sasa ya Bongofleva anayeweza kukufikia,” ni kauli ya mtu ambaye kwa miaka 28 mikono yake imetengeneza baadhi ya “biti” kali na za kihistoria za muziki nchini mtayarishaji mkongwe ambaye masikio yake yamesikia sauti nyingi za wasanii waliotoka wakawa maarufu kuliko na walioishia studio, si mwingine bali ni P’ Funky.
 

Hiyo ni kauli inayoweza kuonesha vipaji ambavyo nchi hii inavyo kitaa na jana vilipata fursa kuonekana kwenye platform kubwa iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Taifa Cup Music Challenge.
 

Kwa upande wa Bongofleva wasanii 10 waliowakilisha mikoa yao walingia fainali na kwa upande wa Singlei wasanii wanne waliingia fainali kusaka washindi watatu. Matokeo yakawa hivi kwa jina na mkoa husika: 

Washindi wa Singeli: 
 

1st  Hamza  Juma  Hamza – Morogoro

2nd Abdulkadri Mwana  Kwangaya- Dsm

3rd  Saleh Abas Zuber – Mjini Magharibi

Muziki wa kizazi kipya:

1st  Abisai Kassanga – Pwani

2nd Meshack Ngemela- Mbeya

3rd Asma Athuman na Asnath Athuman- DSm.
 

Kwa upande wa soka, netiboli na riadha mashindano hayo yanafikia Tamati leo mchana na jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Credit – Fullshangwe Blog.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here