.Na Bibiana Ndumbaro
STAMICO yatangaza bidhaa mpya ya Rafiki Briquettes (Mkaa mbadala) katika Maonesho ya biashara yanayofanyika Zanzibar.
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeshiriki katika maonesho ya sita ya bidhaa za viwanda yenye kauli mbiu Tumia bidhaa za Tanzania jenga uchumi wa Tanzania, ili kutoa elimu kuhusu shughuli na bidhaa mbalimbali za STAMICO.
Maonesho haya yalianza tarehe 3 na yanategemea kumalizika tarehe 9 Disemba 2021 na yanafanyika katika viwanja vya Maisara.
Shughuli za STAMICO zimewavutia sana wananchi wa Zanzibar hususani mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes ambao umeonesha kuwa mkombozi kwa wananchi wengi wanaotumia mkaa utokanao na kuni.
Maonesho haya yanafanyika sambamba na kongamno la uwekezaji linalotarajiwa kufanyika tarehe 7 Disemba 2021 katika hoteli ya Golden Tulip .
STAMICO inawakaribisha wananchi kuendelea kuhudhuria kwa wingi banda la STAMICO na mabanda mengine yaliyoko mtaa wa Madini ili kujifunza shughuli zinazofanywa katika sekta ya Madini.
Katika Maonesho hayo STAMICO imetembelewa na viongozi mbali mbali wa kutoka Zanzibar na kutoka Wizara ya Madini. Viongozi wa Wizara waliotembelea ni pamoja na Kamishna wa Madini Dkt. Abdulhaman Mwanga na Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Musa Budeba.
Maonesho haya yamefunguliwa rasmi leo tarehe 6 Disemba 2021 na Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.