Home LOCAL SPIKA EALA: AFRIKA TUNAJIVUNIA AMANI ILIYOPO TANZANIA, RC ARUSHA: TOKENI NA...

SPIKA EALA: AFRIKA TUNAJIVUNIA AMANI ILIYOPO TANZANIA, RC ARUSHA: TOKENI NA MALENGO YATAKAYOFANYA MTAJWE MIAKA 60 IJAYO

 


NA: NAMNYAK KIVUYO ARUSHA.
Spika wa Bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga amesema kuwa  Afrika nzima inajivunia amani iliyopo Tanzania kwani amani ni msingi wa kila kila kitu ikiwemo maendeleo ya kiuchumi.

Mh Ngoga aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kimkoa katika eneo la makumbusho jijini Arusha ambapo alisema kuwa majirani wanafurahia  mafanikio ya Tanzania kwasababu kipindi cha kutafuta  uhuru Hayati MwalimuJulius Kambarage Nyerere alitamani nchi zote za Afrika zipate uhuru kwa wakati mmoja.

Alisema kuwa kwa amani iliyopo Tanzania ni rahisi kujadili Mambo mengine ya kimaendeleo ndio maana mpaka sasa wamepiga hatua katika sekta mbalimbali tofauti na awali kabla ya uhuru.

“Mwalimu Nyerere wakati Tanzania inapata uhuru alitamani kusimamisha tukio hilo ili nchi za afrika zipate uhuru kwa pamoja kwa hiyo sio muasisi kwenu tu bali na kwa nchi nyingine Afrika ndio mana tunafurahia mafanikio yenu lakini pia ukiwa na amani mambo mengine ni  rahisi mnaona uchumi umekuwa, sekta ya usafiri imekua, huduma za afya zimeboreka elimu iko juu ila  msibweteke hakikisheni mnaenzi na kutunza amani na uhuru waliyojenga waasisi isiingie doa,” Alisema Ngoga.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa watanzania wasilewe bali wayaenzi yaliyofanywa na waasisi kwani mtihani walionao ni kujiuliza je miaka 60 ijayo Kuna watu watakuwa wawaimbe kama hivi sasa wanavyowaimba waasisi.

Alisema kila mmoja aweke lengo atakumbukwajr baada ya miaka 60 ijayo kwani kila mmoja ana nafasi ya kufanya jambo litakalo acha alama katika jamii na nchi kwa ujumla  hivyo katika kusherhekea miaka 60 ya uhuru kila mmoja atoke na lengo la atafanya nini ili kuchangia maendeleo ya familia yake, jamii na nchi kwa ujumla.

“Maendeleo yanakuja kila mmoja ahakikishe anashiriki kikamilifu ili miaka 60 ijayo na sisi tutajwe kwa mema tuliyofanya kwaajili ya nchi yetu kama hivi sasa tunavyowataja waasisi wetu ni ukweli usiopingika kuwa kabla ya uhuru kulikuwa na shule kwaajili ya watoto wa watu maalum tu lakini hivi sasa hakuna ubaguzi shule ni kwaajili ya watanzania wote bila kujali hali ya familia, kabila wala dini,”alisema Mongela.
 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here