Home SPORTS SIMBA, YANGA HAKUNA MBABE

SIMBA, YANGA HAKUNA MBABE


Na: Stella kessy, DAR ES SALAAM.

YAMETIMIA, hatimaye  mechi ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kwa timu zote mbili Simba na Yanga leo zimetoka sare 0-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Huku dakika zimekamilika na ngoma kuwa nzito kwa timu zote ambapo zimegawana pointi mojamoja.

Mpaka mwamuzi wa kazi Herry Sasii anapulizi kipyenga cha mwisho hakuna mbabe kwenye mchezo huo.

Hata hivyo Yanga inaendelea na rekodi yake ya kucheza mechi ya nane bila kufungwa huku Simba ikikwama kuivunja rekodi ya Yanga ya kucheza mechi zake bila kufungwa.

Adha timu hiyo ya Jangwani imeendelea kuwa vinara wa ligi kuu kwa kufikisha pointi 20 nafasi ya kwanza, na timu ya Simba kiwa na pointi 18 na kushika  nafasi ya pili

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here