Home SPORTS SIMBA YAFUZU MAKUNDI,SHIRIKISHO

SIMBA YAFUZU MAKUNDI,SHIRIKISHO

 

Mwandishi wetu

MABINGWA wa Tanzania bara Simba leo wamefanikiwa  kutinga hatua ya makundi  Kombe la Shirikisho Afrika .

Katika mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Heroes,Zambia dakika 90 zimekamilika kwa ubao kusoma Red Arrows 2-1 Simba ambapo bao la Simba lilifungwa na kiungo Hassan Dilunga.

Dilunga aliweza kufunga  bao hilo akiwa ndani ya 18 baada ya beki wa Red Arrows kufanya uzembe kwenye kuokoa mpira mrefu uliopigwa na kiungo, Rally  Bwalya ilikuwa dakika ya 67.

Mabao ya Red Arrows  yalifungwa na Eric Banda dakika ya 44 kwa shuti kali na lile la pili lilifungwa na Joesph Phiri dakika ya 46 kwa kichwa kilichowashinda mabeki.

Simba inasonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2 kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba ilishinda mabao 3-0 ambayo yalifungwa na Bernard Morrison aliyetupia mawili lakini leo alibanwa na wapinzani wake pamoja na Meddie Kagere huyu alitupia bao moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here