Home LOCAL SERIKALI YAPOKEA DOZI 115,200 ZA JANSSEN.

SERIKALI YAPOKEA DOZI 115,200 ZA JANSSEN.




 

Na: WAMJW-DSM

Tanzania imepokea shehena ya Chanjo ya Janssen Dozi 115,200 kutoka Serikali ya Ubeligiji kupitia mpango wa COVAX Facility utaosaidia kuchanja wananchi 115,200 ili kuwakinga dhidi ya  UVIKO-19.

Akizingumza na waandishi wa habari katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam baada ya kupokea Chanjo kutoka kwa Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania Peter Van Acker Dkt. Gwajima amesema kuwa, Serikali itaendelea kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 katika vituo mbalimbali vya Afya ili kuwakinga Wananchi.

Amesema kuwa, awamu ya kwanza Serikali ilipokea dozi 1,058,400, awamu ya pili dozi 169,000 na leo Desemba 3, 2021 hivyo kufanya jumla ya Chanjo aina ya Janssen zilizopokelewa hapa nchini kufikia Dozi 1,342,600 na kufanya jumla ya chanjo zote zilizopokelewa kuwa  dozi 4,421,540 zikiwemo chanjo ya Sinopharm na Pfizer ambazo zitachanja watu 2,882,545 .

Aidha Dkt Gwajima amewaagiza viongozi na watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhamasisha jamii kujitokeza kupata chanjo na  kisha kujikinga kwa kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko 19 ikiwa ni pamoja na uvaaji wa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kutumia vitakasa mikono (Sanitizer), kufanya mazoezi na kuepuka misongamano isiyo yalazima.

Mwisho.

Previous articleWAZIRI GWAJIMA AZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA UVIKO-19 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM.
Next articleTAMKO LA THUB WAKATI WA MAADHIMISHO YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here