Home LOCAL RAIS MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI, YUMO CHARLES MARTIN HILLARY

RAIS MWINYI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI, YUMO CHARLES MARTIN HILLARY

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi wafuatavyo.

Mosi, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Charles Martin Hillary kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Pili kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said leo Desemba 30,2021 pia Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Yusuph Majid Nassor kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS).

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Idrissa Muslim Hija kuwa Mwenyekiti wa Bodi Uhaulishaji Ardhi Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza leo Desemba 30,2021.

Previous articleIBRAHIM AJIBU AMWAGA WINO AZAM FC
Next articleNHC YABUNI TEKNOLOJIA MPYA YA VITASA JANJA, KUANZA NA WADAIWA SUGU JANUARY
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here