Home SPORTS PABLO: WACHEZAJI WOTE WAKO FITI

PABLO: WACHEZAJI WOTE WAKO FITI

Na: stella kessy

KOCHA Mkuu wa klabu ya Simba Pablo Franco  ameweka wazi kuwa wachezaji wake wapo vizuri kuelekea mechi dhidi ya KMC utakochezwa katika dimba la Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.

Amesema kuwa katika muda wa siku sita zilizopita wachezaji wake waliugua hivyo hawakupata nafasi ya kufanya maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya KMC.

Amesema kuwa baadabya kuwasili Mkoani Tabora kikosi kilifanya mazoezu kamoli kuelekea mechi yenyewe hivyo hawakujiandaa vizuri.

Amesema kuwa kutokana na changamoto hiyo amewaandaa wachezaji kimwili kiakili kwa ajili ua mchezo huo ambao wanatarajia utakuwa mgumu.

“Hatukupata mida mrefu wa kujiandaa kutokana na changamoto ya ugonjwa iliyowapata wachezaji wangu, jana ndi tulifanya mazoezi ya kuweka miili sawa baada ya kufika Tabora ila tumefanya mazoezi ya mwisho.

Aliongea kuwa sababu hawana mamlaka ya kusogeza mbele mechi yao dhidi ya KMC kwani kikosi bado hakipo sawa kuelekea mechi hiyo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here