Home SPORTS PABLO ARIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

PABLO ARIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco amesema kuwa amefurahishwa na kiwango cha wachezaji wake kijituma muda wote katika mchezo wao dhidi ya wapinzani wao Yanga.

Amesema wachezaji walijitoa kwa hali zote kuhakikisha wanapata ushindi.

Ameongeza kuwa licha ya kupata siku mbili za kufanya mqzoezi baada ya kurudi kutoka Zambia lakini wachezaji walijitaidi kuafuata maelekezon.

“Najivunia kufanya kazi na wachezaji wa kikosi changu wamefanya kazi kunwa kila mmoja alitimiza vema majukumu yake uwanjani” amesema.

“Siwezi msifia mchezaji mmoja mmoja bali ni timu mzima, tulizuia kwa pamoja na kishambulia kwa pamoja kilichotokea ni bao la ushindi kwa kugawana point ” alisema

Aliongeza kuwa kikosi kimeingia leo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya tatu ya maichuano ya Azam Sport Federation Cup (ASFC) dhidi ya Jkt Tanzania utakaocheza kesho.

Wachezaji wote wataingia kambini  huku wale ambao wanaendelea kupona majeraha yao nao wakiwepo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here