Home SPORTS NAIBU WAZIRI GEKUL AWAALIKA WADAU KUONA VIPAJI MASHINDANO YA TAIFA CUP

NAIBU WAZIRI GEKUL AWAALIKA WADAU KUONA VIPAJI MASHINDANO YA TAIFA CUP

NA:STELLA KESSY

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amevitaka  vyama vya michezo na shirikisho kujitokeza kwa wingi kuona vipaji  katika michuano ya taifa cup inayotarajiwa kuanza Desemba 10 mwaka huu.

Akizungumza leo katika drooo ya michuana hiyo Naibu waziri amesema kuwa katika michuano hiyo vipaji ni vingi kwani wachezaji wengi kutoka katika mikoa taofauti wamethibitisha kushiriki.

Amesema kuwa jumla ya mikoa 16 imethibitisha kushiriki katika michuano hiyo ambayo leo wamepata makundi kwa kila mkoa inajua mpinzani wake.

“Sintapenda kuona vipaji vya michezo vinaishia hapa kwani naomba vyama vya michezo pamoja na shirikisho kujitokeza kwa wingi katika michuano hiyo ili kuendeleza vipaji vya washiriki.

Aliongeza kuwa serikali ga awamu ya sita imelenga kuinua vipaji vya michezo yote hapa nchini kwani Tanzania ni nchi iliyobarikiwa na ina vipaji vingi vya michezo.

Amesema kuwa michezo ni sehemu ya afya na kuwataka mikoa iliyoshiriki katika michuano hiyo inatakiwa kuonyesha ushirikiano katika michuano  hiyo.

“Naomba mikoa ambayo imethitibisha kushiriki inatakiwa kuonyesha umoja katika michuano hii kwani taifa linahitaji vipaji vya kutosha lakinj sasa michezo imekuwa mingi hapo awali mchezo ulikuwa moja lakini sasa michezo imekuwa mitatu mpira wa miguu kwa wanaume na wanawake, riadha na mpira wa pete”

Previous articleMOBETO HQ WAMWAGA ZAWADI YA SIKUKUU KWA WANAWAKE
Next articleWACHEZAJI WANNE AZAM FC KUIKOSA MECHI YA KAGERA SUGAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here