Home SPORTS NAIBU WAZIRI GEKUL ATOA NENO KWA TIMU ZA TANZANIA MPIRA WA MIKONO

NAIBU WAZIRI GEKUL ATOA NENO KWA TIMU ZA TANZANIA MPIRA WA MIKONO

 



Na: Stella Kessy, DAR.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amezitaka timu za Tanzania  ambazo hazikufanya vizuri katika mashindano   ya  Mpira wa Mikono Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kujipanga kwa mwakani.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifunga michuano hiyo  iliyokuwa inafanyika katika  Uwanja wa Ndani wa Taifa ,Dar Es Salaam.

Amesema kuwa serikali imelenga kuinua michezo na wameanzisha mfuko kwa ajili ya kuinua michezo hapa nchini.

“Raisi wetu mama  samia amelenga kuinua michezo hivyo nawaomba sana watanzania kama leo mmeshindwa jiandae kwa ajili ya mwakani kwani kuna mfuko ambao umelenga kuinua michezo hapa nchini”amesem.

Aidha amewapongeza wachezaji na timu zilizoshiriki katika michuano hiyo na kuomba kwa umoja walioonyesha na kushirikiana katika kutafuta mshindi wa michuano hiyo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mikono Tanzania(  TAHA) Michael Chibawala,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa jitihada  ya kuinua michezo hapa nchini.

Hata hivyo katika  mashindano hayo  yameshirikisha Klabu 11 kutoka nchi ya Kenya ,Rwanda na Tanzania wenyeji.

Amesema kuwa lengo ni kupata Klabu nne za juu,mbili Wanawake na mbili wanaume watakaofuzu kushiriki mashindano ya Vilabu Afrika yatakayofanyika mwakani.

“Maandalizi yapo vizuri lakini tulitarajia kuwa na Klabu 19  kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zingine zimeshindwa kufika kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo,hivyo kwa walioshiriki tunatarajia kuona ushindani na kutimiza malengo tuliokusudia,” alisema Chibawala.

Alitaja klabu nyingine shiriki ni ya wanaume  Black Mamba(Kenya)Polisi Rwanda, Ngome (Tanzania), na Nyuki  (Zanzibar),  huku wanawake Kizugiro(Rwanda)  na  Ngome(Tanzania).

Wakati huo huo mshindi wa kwanza aliibuka  polisi rwanda kwa wanaume huku kwa upande wa wanawake ni Nairobi water wamepata kombe na Medali.

Nafasi ya pili imeshikiliwa  Cereals wanawake na wanaume kutoka Kenya  wamepata kombe na medali, huku Black Mamba wakimalizia nafasi ya tatu ,wakati upande wa wanawake   Kiziguro Rwanda wamekamata nafasi ya tatu.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here