Home SPORTS NABI: APONGEZA TIMU ZOTE MBILI KWA MCHEZO MZURI

NABI: APONGEZA TIMU ZOTE MBILI KWA MCHEZO MZURI

Na: Stella Kessy, DAR

KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga Nasradine Nabi, amesema kuwa wapinzani wao simba wapo imara na ndio maana wameshindwa kupata matokea katika mchezo wa juzi.

Akizungumza baada ya mechi kuisha kocha huyo amesema kuwa  kikosi cha simba kimekuwa imara tofauti na kipindi kile ambacho yupo Didier Gomes.

“Mchezo ulikuwa mzuri na ulitawaliwa na mbinu nyingi na ndio maana hakukuwa na nafasi nyingi japo tulicheza  vizuri kipindi cha kwanza na Simba ikacheza vizuri kipindi cha pili na kutengeneza nafasi ambayo hazikuwa na matuta.”

“wapinzani wetu wameimarika na tulichofanya ni kuwazuia wasipate nafasi ya kufunga “ amesema

Pia  aliweka wazi kwamba hakukuwa na timu ambayo ilikuwa na uhakika wa kupata ushindi kwenye mchezo huo. 

“Awali niliweka wazi kwamba mchezo wetu wa dabi ni nusunusu kwa kila timu kupata ushindi na imetokea hivyo hakuna wa kumlaumu kwa kuwa ni mpira.

“Naweza kusema kwamba hatukutumia nafasi ambazo tulizitengeneza kwenye mchezo wetu na hilo limetufanya tushindwe kupata ushindi lakini wachezaji walicheza vizuri,” amesema.

Yanga inafikisha pointi 20 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 18 baada ya kucheza mechi nane.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here