Home ENTERTAINMENTS MOBETO HQ WAMWAGA ZAWADI YA SIKUKUU KWA WANAWAKE

MOBETO HQ WAMWAGA ZAWADI YA SIKUKUU KWA WANAWAKE


NA: MWANDISHI WETU.

MWANAMITINDO mkongwe nchi Hamisa Mobeto, ambaye ni balozi wa taulo za kike katika kampuni ya HQ , amezindua ongezeko la taulo mbili katika kifungashio kimoja.

Huu ni mwaka wa kumi tangu kampuni hii ianze kutoa huduma ya  taulo za kike  hapa nchini ambapo awali zilikuwa pisi nane na sasa itakuwa 10 kwa kila paketi.

Akizungumza na waandishi wa habari Hamisa Mobeto, amesema hii ni zawadi ya sikuku ambayo itadumu kwa muda wote kwa watumiaji wa taulo hizo zenye ubora wa juu.

“Ongezeko la pisi mbili sio kwa sababu kuna utofauti wa ubora lahasha ubora upo vile vile sababu ya kuongeza ni kurudisha shukurani kwa watumiaji wetu kwa kipindi cha miaka 10 tulodumu sokoni,” anasema Mobeto.

Kwa upande wa muakilishi wa kampuni hiyo amesema wamekuwa wakitembelea shule za msingi kwa ajili ya kutoa elimi kwa watoto wa kike wanao pevuka pamoja na kuwapatia taulo hizo.

“Kwa kipindi cha mwaka huu tumefanikiwa kufikia shule zaidi ya mia moja zilizopo  jijini Dar es Salaam na kuzungumza na watoto wa kike juu ya utumiaji wa bidhaa yetu na kutoa ushauri mbalimbali.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here