Na: Stella Kessy
MABINGWA wa Tanzania simba leo wanashuka dimbani kuchuana na Red Arrows katika mechi ya marudiano ya michuano kombe la shirikisho Afrika huko utaochezwa nchini Zambia.
Kikosi cha simba kinashuka dimbani katika mchezo huo ikiwa na idadi ya mabao 3 dhidi ya wapinzani wao.
Kikosi hicho kimesafiri na wachezaji 25 na jana wamefanya mazoezi na tayari wachezaji wapo tayari kwa mechi.
Kwa upanda wa kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco amesema kuwa katika mchezo wa leo wachezaji wake wanatakiwa kuwa makini na kutumia nafasi àmbazo watapata.
Huku amewataka wachezaji kutumia nafasi ambazo watapata dhidi ya wapinzani wao.
Aidha ameongeza kuwa angependa kuingia katika hatua yq makundi kwa ushindi hivyo amewataka wachezaji kutumia vyema nafasi itakayopatika na Walinzi nao kuwa makini kuwazuia Red Arrows.
“Nategemea mchezo utakuwa mgumu tunajua wataingia kwa kishambulia kuanzia mwanzoni lakini nisingienda kufuzu hatua inayofuata kwa kipoteza.
Amefafanua kuwa anatambua klabu yake ni kubwa na ina wachezaji bora ambao hawatamuangusha katika mchezo huu