Home LOCAL MDH YATOA VIFAA KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

MDH YATOA VIFAA KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

 

 
Mratibu wa Shirika la usimamizi na uboreshaji wa huduma za afya(MDH)mkoa wa Ruvuma Dkt Nikson John kulia,akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Tunduru Dkt Mussa Chaula, vifaa mbalimbali vya kukusanyia sampuli za makohozi ambavyo vitatumika katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu wilayani humo,anayeshuhudia kushoto ni Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya hiyo Dkt Mkasange Kihongole.

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Dkt Mussa Chaula kulia,akimkabidhi muhudumu wa afya ngazi ya jamii Maria Komba vifaa mbalimbali vya kukusanyia sampuli za makohozi vilivyotolewa na Shirika la usimamizi na uboreshaji wa huduma za Afya(MDH)kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa kifua Kikuu wilayani humo,katikati mratibu wa kifua Kikuu na Ukoma wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole.

Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole akizungumza na baadhi ya waganga wa tiba asili tiba mbadala wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa waganga hao juu ya ugonjwa wa kifua kikuu kabla ya kushirikishwa katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa huo ambapo zaidi ya waganga wa tiba asili 50 wamepata mafunzo hayo.

Na: Muhidin Amri, Tunduru

HOSPITALI ya wilaya Tunduru mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na shirika la usimamizi na uboreshaji wa huduma za afya(MDH)imezindua mkakati wa kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu kwa kutoa  vifaa vya kukusanyia sampuli za makohozi kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Mratibu wa MDH Dkt Nikson John alisema, vifaa hivyo vilivyotolewa  kwa wahudumu wa afya ni kuunga mkono juhudi za Serikali  na zinalenga kusaidia katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa huo ambao bado umekuwa tatizo kwa jamii hasa wanaoishi maeneo ya pembezoni.

Dkt Nikson alisema,MDH mkoa wa Ruvuma  inasaidia eneo la kifua kikuu kwa kutoa vifaa na kuwawezesha wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu ambapo amevitaja vifaa  hivyo ni wahudumu hao ni makoti ya mvua,buti, na vifaa vya kukusanyia sampuli za makohozi.

Alisema, vifaa hivyo vinakwenda kuongeza hamasa kwa wahudumu hao pamoja na kuleta tija katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu inayofanywa na Hospitali ya wilaya kupitia kitengo cha kifua kikuu na ukoma.

Kwa upande wake,Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole amewashukuru wadau Shirika la MDH kwa kutoa vifaa ambavyo vitasaidia katika kampeni ya  kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu hasa wakati huu wa masika ambapo Jiografia ya wilaya hiyo sio rafiki kwa wahudumu hao ambao wanakwenda katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao.

Alisema, vifaa hivyo vitawapa morali wahudumu  hao  kwa kufanya kazi katika mazingira yoyote bila kujali mvua  au jua ambapo lengo la wilaya hiyo ni kufanya vizuri katika mapambano ya ugonjwa wa  huo chini ya kauli mbiu kila unayemuona mbele yako ni “muhisiwa wa kifua kikuu”.

Alisema, vifaa hivyo  vilivyotolewa katika kitengo cha kifua kikuu na ukoma vitaleta ufanisi  mkubwa kwa kuibua wahisiwa wengi, kwani unapopata  idadi kubwa ya wahisiwa ni dhahiri hata wagonjwa wataongezeka.

Dkt Kihongole alisema,lengo la wilaya hiyo ni kuendelea kuibua wagonjwa wengi ambao wataanzishiwa  matibabu  ili wilaya  ya Tunduru ibaki salama bila maambukizi ya ugonjwa huo.

Naye muhudumu wa afya ngazi jamii Iddi Yakiti(Nyuki) amelishukuru Shirika la MDH kwa kutoa vifaa hivyo ambavyo vinakwnda kusaidia katika kazi ya kukusanya sampuli za makohozi vijijini na kuleta vituoni kwa ajili ya uchunguzi.

Alisema, awali utendaji wa majukumu yao ulikuwa mgumu kwani wakati mwingine walinyeshewa na mvua na kusababisha hata sampuli za makohozi nazo kulowa jambo lililosababisha kushindwa kufikia malengo yao.
MWISHO.

Previous articleMZEE KIMITI AWATAKA WANA RUKWA KUIUNGA MKONO SERIKALI
Next articleMHE. HAMAD HASSAN CHANDE AFANYA ZIARA YA KIKAZI TEA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here