Home ENTERTAINMENTS MBINIFU MKONGWE WA MAVAZI JOKTANI ATAMBA KUTIKISA ZANZINZAR

MBINIFU MKONGWE WA MAVAZI JOKTANI ATAMBA KUTIKISA ZANZINZAR

 

NA: MWANDISHI WETU

MBUNIFU mkongwe wa mavazi ya asili Joktani Makeke ametamba kutikisa katika tamasha la mavazi Runway Bay, kisiwani Zanzibari.

Tamasha hilo litaanza Desemba 26, mpaka 29 litaanziaa Old Fort Ngome Kongwe, siku ya pili Sea Front Mizingani, siku ya tatu Marumaru hoteli, kilele kitafanyika Living Stone.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema ameandaa mavazi ya utamaduni mapya ambayo hayajawahi kuonyeshwa sehemu na mbunifu yeyote.

“Nipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya mavazi ambayo nitaonyesha katika tamasha la Runway Bay, nguo za jinsia zote wabunifu wenzangu wajipange kwa sababu nimepanga kufunika jukwaaa,” anasema Makeke.

Mbalimbali  na maonyesho ya mavazi kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa ndani na nje ya Tanzania, na utoajia wa tuzo kwa wadau wa mitindo waliofanya vizuri.

Kwa upande wa muasisi wa jukwaa hilo Waiz Houston Shelukindo, amewaomba wadau kujitokeza katika tamasha hilo ambayo kiingilio ni dola 35 za kimarekani kwa siku zote.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here