Home SPORTS MATOLA: KIKOSI KIPO KAMILI KWA GEITA GOLD

MATOLA: KIKOSI KIPO KAMILI KWA GEITA GOLD

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu simba leo wanashuka dimbani kuchuana na Geita Gold katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara katika dimba la Uwanja wa Benjaminj Mkapa Jiji Dar  es salaam.

Kikosi cha simba kinashuka dimbani kikiwa kibabe baada ya mechi yake ya mwisho dhidi ya Ruvu shooting kutoka na ushindi wa bao 3-0.

Katika mchezo uliopigwa katika dimba la CCM kirumba mkoani mwanza huku simba wakiwa wageni katika mchezo huo.

Kuelekea mchezo huo kocha msaidizi wa kikosi hicho Seleman Matola amesema kuwa  mchezo huo dhidi ya Geita utakuwa mgumu kwani wataingia kwa tahadhari ikiwemo kuwaheshimu wapinzani wao na kuhakikisha wanajinyakulia point 3 dhidi yao.

“Geita si timu mbaya ipo vizuri na tunaiheshimu, tunaingia uwnajani tukiwa na tahadhari zote tunahitaji kupata alama zote tatu, wachezaji  wote wapo kambini tayari kwa mchezo”amesema Matola

Ameongeza kuwa maandalizi yamekamilika wachezaji walipata siku mbili za kufanya mazoezi baada ya machezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi Red Arrows, jumapili iliyopita.

Wachezaji wote wapo kambini na wamefanya mazoezi ya mwisho hivyo benchi la ufundi litakuwa wa wigo mpana wa kuchagua kikosi kitakachoshuka  uwanjani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here