Home SPORTS MASHABIKI WA YANGA SC WAMIMINIKA KUCHANGIA DAMU MOI, WAKUSANYA CHUPA ZAIDI 100

MASHABIKI WA YANGA SC WAMIMINIKA KUCHANGIA DAMU MOI, WAKUSANYA CHUPA ZAIDI 100

 




Na: Mwandishi Wetu.
 
MASHABIKI na Wanachama wa Klabu yenye maskani yake mitaa ya Jangwani na Twiga, Yanga Africans SC wamejitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa watu wenye uhitaji katika Taasisi ya Mifupa (MOI) na kuchangia chupa zaidi 100.

Awali Mkurugenzi wa Tiba wa MOI, Dk. Samuel Swai alipongeza uongozi wa Klabu hiyo ya Yanga kwa kuendelea kuwaunga mkono kwa kuratibu zoezi hilo la uchangiaji damu kwa kutoa jezi kwa kila ayeshiriki.

“Wamekuwa wakiunga mkono zoezi la uchangiaji wa damu kwa mashabiki wao wa Yanga kufika kwa wingi na hii ni mara ya Nne kufanya hivi”. Alisema Dk. Swai.

Dk. Swai amebainisha kuwa, damu hiyo ni maalum kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi wa ajali wanaotibiwa katika hospitali hiyo. 

“Tunawashukuru wadau  GSM na Yanga kwa kutuunga mkono kwenye zoezi hili.limeenda vizuri na wamemiminika wachangia damu  wengi na kukusanya chupa zaidi ya 100.” Alisema Dk. Swai.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Yanga, Hersi Said ambaye nae alipata wasaha wa kuchangia damu pamoja na mashabiki na wanachama wa Yanga, alisema kuwa mbali na masuala ya mpira uwanjani pia wanarejesha fadhira kwa jamii ikiwemo kufanya shuguli za uchangiaji damu.

“Ni furaha ya kutimiza miaka 60 na pia kuelekea mchezo wa watani wa jadi.
Tumefanya zoezi hili kusaidia jamii yenye uhitaji.

Hersi aliongeza kuwa, zoezi la uchangiaji damu limefanywa na wana Yanga ambao wameweza pia kupata zawadi za jezi  ya timu yao ya Yanga.

Pia katika tukio hilo, Mkurugenzi mkuu wa Yanga, Bw. Senzo Mazingiza nae alipata wasaha wa kuchangia damu pamoja na kutoa zawadi za jezi kwa mashabiki waliofika kuchangia damu wa zoezi hilo 

Kwa upande wake Ofisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi aliwashukuru watu mbalimbali waliojitokeza kuchangia damu kwani imekuwa ikiwapa faraja kama uongozi wa MOI kwani mahitaji kwa kila siku ni mengi.

“Mpaka zoezi linakwisha jioni tumeweza kupokea chupa zaidi ya 100 za damu.

MOI inapokea watu wengi wakiwemo wa majeruhi. Wenye ndugu na wasio na ndugu. 
Pia kuna wahitaji wa damu kwa kila zoei la upasuaji mkubwa kwenye vitengo vyetu ndani ya MOI.

Wadau wengine pia wanakarobishwa kwa wingi katika kuchangia damu kuokoa watu.” Alimalizia Mvungi.

Klabu ya Yanga SC kesho wanatarajiwa kushuka dimbani wakiwa wageni dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here