Na: Mwandishi wetu.
KOCHA wa Coastal Union, Melis Medo, amewashauri wachezaji wake kuchomwa chanjo ya ugonjwa Corona ili kujingika na ugonjwa.
Medo alifanya kikao na wachezaji wake pamoja na benchi lake la ufundi jana na kutoa ushauri huo ambao ulipokelewa vizuri.
Amesema ni bora kuchukua tahadhari kuliko kuendelea wakati afya ni kitu muhimu ambayo bila kuwa nayo huwezi kucheza mpira.
“Najua wengi wenu hamna imani ni hizi chanjo, lakini ni bora kuwa na hata asilimia 50 ya kinga kuliko kupambana na Corona bila ya kuwa na kinga,” alisema Medo
Ameongeza kuwa vidudu vya Corona kwa sasa vimekuwa vya tofauti sana kwa kuwa unaweza ukapima ukakutwa na malaria au UTI ukatumia dawa usipate nafuu.
Katika kikao hicho kilichofanyika Musoma walikokwenda kucheza na Biashara United na kushinda 1-0, wachezaji waliridhia ushauri huo na kupanga kwenda kuchanjwa watakaporejea Tanga.
Kikosi hiko kinachoshika nafasi ya tano kikiwa na pointi 14, kiliondoka jana usiku Musoma kurejea Tanga kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao mwingine wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani.