Home SPORTS KMC YAIPIGIA HESABU RUVU SHOOTING

KMC YAIPIGIA HESABU RUVU SHOOTING


Na: Stella Kessy, DAR ES ASALAAM.

KOCHA Msaidizi wa Klabu ya KMC Habib Kondo, amesema kuwa kwasasa hesabu yao ni kupata pointi tatu dhidi ya  Ruvu Shooting.

KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na kuwafanya wayeyushe pointi tatu mazima.

Leo KMC itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

“Matokeo ya mchezo wetu uliopita tumesahau kwa kuwa hayawezi kubadilika na badala yake tunautazama huu uliopo mbele yetu dhidi ya Ruvu Shooting.

“Hautakuwa mchezo mwepesi kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi lakini ni muhimu kwetu kupata pointi tatu,” amesema.

KMC ikiwa imecheza mechi 10 imekusanya pointi 10 inakutana na Ruvu Shooting iliyokusanya pointi 9 baada ya kucheza mechi 10.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here