Home SPORTS KLABU YA SIMBA YAZINGUA RASMI KAMPENI YA KUCHANGIA FEDHA ZA KUJENGA UWANJA...

KLABU YA SIMBA YAZINGUA RASMI KAMPENI YA KUCHANGIA FEDHA ZA KUJENGA UWANJA WAKE



NA: STELLA KESSY

KLABU  ya simba leo imezindua rasmi kampeni ya kuchangia fedha za kujenga uwanja wa kisasa kwa ajili ya mechi za nyumbani.

Hatua hiyo imekuja  siku chache baada ya mwekezaji wa klabu, Mohammed Dewji aliishauri bodi ya wakurugenzi kutanganza utaratibu wa kuchangisha wanachama na mashabiki huku yeye akiahidi kutoa bilioni 2 kufanikisha ujenzi huo.

Akizungumza na waandishi wa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez amesema kuwa lengo lao kubwa simba ni kujenga uwanja  ambapo mwezi wa kwanza watatoa ramani ambayo itaonyesha jinsi ya uwanja utakavyokuwa.

“leo tumezindua kampeni ya kujenga uwanja ambayo inasema tumeamu,tunaweza,simba  yetu,kiwanja chetu,najua simba haijashindwa kujenga uwanja ila tunataka kila mwanachana aweze kuchangia ujenzi wa Uwanja”alisema

Aliongeza kuwa kwasasa simba ina malengo na nia ya kujenga uwanja kwa kupitia nguvu za wananchi.

Amesema kuwa kwa wale wadau na wapenzj wa simba wanatakiwa kushirikiana kwa nguvu moja ili kufanikisha lengo hilo.

Kwa upande wa Mangugu alisema kuwa hili ni jambo muhimu kwa wanachama Mfumo rasmi wa kuchangia.

Mwenyekiti wa klabu ya simba Mutraza Mangungu   wamezingua kampeni hiyo leo  inayoitwa ‘Simba yetu Uwanja Wetu’kwa ajili ya kuhamasisha watu kuchangia.

Wanachama na mashabiki watachangia pesa kutipita mtandao wa simu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here