Home SPORTS KIKOSI CHA YANGA KUIFUATA PRISONS

KIKOSI CHA YANGA KUIFUATA PRISONS

Na: Mwandishi wetu.

MABINGWA wa kihistoria Yanga  leo mchana kinaondoka kuelekea  Sumbawanga kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons, huku ikiwakosa nyota wake wanne kutokana na kuwa majeruhi, akiwamo beki kiraka Kibwana Shomary.

Mbali na Kibwana, wengine waliobakizwa Dar ni Yacouba, Yusuf Athuman na Mapinduzi Balama na Meneja wa Yanga Hafidh Saleh alisema wengine waliosalia wapo fiti akiwamo Fiston Mayele ambaye juzi kwenye mechi ya ASFC dhidi ya Ihefu aliishia kukaa jukwaani.

Yanga inavaana na Prisons huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote katika mechi zao nane za Ligi Kuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here