Home LOCAL KESI YA DC WAZAMANI TABORA KUANZA KUUNGURUMA DISEMBA 17, 2021

KESI YA DC WAZAMANI TABORA KUANZA KUUNGURUMA DISEMBA 17, 2021

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya

Na: Lucas Raphael,Tabora

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Wialaya ya Tabora inayosikiliza Kesi ya Madai ya Fidia ya Zaidi ya shilingi 100 milioni inayomkabili Kitwala Komanya Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya imepangwa kusikiliza shauri hilo Desemba 17 mwaka huu.

Uamzi huo umefikiwa jana na Hakimu Nzige Sigwa baada ya Mdaiwa Komanya kuwasilisha ombi la kusogezwa mbele shauri hilo kwa vile Wakili wake Issa Mavula yupo safari ya kikazi Jijini Dar ess salaam.

Kufuatia maombi hayo kufikishwa mahakamani bila ya Mdaiwa Komanya kuwepo wakili wa mlalamikaji Kelvin Kayaga aliiomwomba hakimu atoe hailisho la mwisho kwani shauri hilo limechukua mda mrefu.

Hakimu Sigwa mara baada ya kupokea hoja za pande hizo amepanga kuanza kusikiliza shauri hilo la madai namba 04/2021 ambapo mdai Alex Tonge anadai alidhalilishwa na Komanya wakati huo akiwa ni mkuu wa Wilaya ya Tabora hivyo alipwe fidia ya shilingi milioni 140.

Komanya ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mara ya mwisho alipanda Kizimbani Novemba 17/2021 bila kuwa na wakili wake na kuiomba Mahakama ianze kusikiliza shauri hilo Desemba mosi mwaka huu.

Mdai katika Shauri hili Alex Ntonge kupitia kwa wakili Kelvin Kayaga anadai alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa na Komanya Januari 05/2021.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo Komanya ambaye wakati huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askali wa jeshi la Polisi walifika nyumbani kwake na Kumdhalilisha.

Aliongeza kuwa Mkuu huyo wa Wilaya aliyeenguliwa akiwa na askali wenye Silaha baada ya kufika nyumbani hapo walimkamata mdai Ntonge na kisha walimfanyia vitendo vinavyodhalilisha utu wake mbele ya familia yake na majirani zake.

Shauri hilo la madai dhidi ya Mkuu wa Wilaya aliyeenguliwa na Rais Samia Suluhu Juni 19 mwaka huu msingi wake unatokana na udhalilishaji.

MWISHO.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here