Home LOCAL JESHI LA POLISI LA KAMATA JEZI FEKI

JESHI LA POLISI LA KAMATA JEZI FEKI

 

Ndugu wanahabari,

Jeshi la Polisi lingependa kuzungumzia juu ya tatizo la uuzaji wa jezi feki zinazotumiwa na timu mbalimbali za hapa nchini.

Kwanza Jeshi la Polisi linasema  utengenezaji na uuzaji wa jezi feki  (zisizo na kiwango) ni kosa la jinai na kibaya zaidi wanaofanya hivyo wanakuwa wakikwepa kulipa kodi kwa sababu hazipitii katika mfumo ulio rasmi.

Ndugu wanahabari,

Kama mnavyofahamu baadhi ya timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huingia mikataba na kampuni mbalimbali ya kutengeneza jezi na pale zinapouzwa kiasi fulani huingia katika timu  ili kugharamia  mahitaji ya wachezaji kama  mishahara.

Timu kama Polisi Tanzania imefanya hivyo kwa kuingia mkataba na baadhi ya kampuni kama vile Lodhia Group of Companies na Kampuni ya Vunja Bei.

Ndugu wanahabari,

Kwa bahati mbaya na kwa nia ovu ya kujipatia fedha  kinyume cha sheria za nchi, baada ya timu hizo kuingia mikataba, utengenezaji, usambazaji na mauzo yanapo anza wapo watu wanaotengeneza jezi zilizo chini ya kiwango (jezi feki) kwa kutumia nembo zilezile na kuanza  kuziuza mitaani. Kwa kufanya hivyo huinyima serikali mapato na kibaya zaidi timu hukosa  fedha zikiwepo za kuwalipa wachezaji. 

Katika  msako ulioendeshwa na Jeshi la Polisi watuhumiwa 15 wameshakamatwa kutoka maeneo ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Tabora na Tunduma ambapo  jumla ya Jezi feki 279, Urembo (ribons) 300 na Kofia 6 zimekamatwa. Kesi zimefunguliwa dhidi yao na upelelezi ukikamilika watafikishwa  mahakamani.

Aidha katika uchunguzi uliofanyika imebainika kuwepo na wafanyabiashara  waliofanya mawasiliano na viwanda vya ndani na nje ambavyo jezi halali hutengenezwa wakitoa oda ya kutengenezewa jezi feki. Hawa nao ambao jumla yao ni 11 wamefunguliwa  jalada, wamehojiwa na ushahidi unaendelea kukusanywa.

Ndugu wanahabari,

Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa watu wanaofanya  hivyo kuacha mara moja kwani watachukuliwa hatua endapo wataendelea kufanya uhalifu huo.

Aidha tunatoa wito kwa timu ambazo zitabaini watu wanaotengeneza na kuuza jezi feki zenye nembo walizokubaliana katika mikataba walioingia na kampuni wasisite kutoa taarifa  kituo chochote cha Polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watu hao.

Pia kwa Watanzania, wanapo nunua jezi za timu wanazozipenda na kuzishabikia, wanunue kwenye maduka stahiki na pale watakapo baini kuuziwa jezi feki wasisite kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi. Wananchi tunaomba watambue jezi hizo feki wanauziwa bei ile ile ya jezi halali, ambazo ukitumia hazidumu kama zile halali.

Tukumbuke tatizo la bidhaa bandia (feki) ni la dunia nzima, tukilifumbia macho hili la jezi feki wahalifu wana tabia ya kunogewa, watahamia hata katika dawa za kutibu binadamu, mifugo na hata katika vifaa mbalimbali vya matumizi ya binadamu na madhara yatakuwa kwetu sote.

Nipende kuwajusha kuwa operesheni na misako endelevu itaendelea nchi nzima kwa Jeshi la Polisi kushirikiana na Makampuni yaliyoingia mikataba na timu na timu zenyewe hadi uhalifu huu utakapo koma.

Aksanteni kwa kunisikiliza.

Imetolewa na: 

David A. Misime – SACP

Msemaji wa Jeshi la Polisi

Makao Makuu ya Polisi

Dodoma, Tanzania

 

Previous articleTAIFA CUP 2021 MUSIC CHALLENGE YAMALIZIKA KWA MIKOA KUTOA MASTAA WAPYA
Next articleWAZIRI UMMY APIGA MARUFUKU KUWASHUSHA VYEO WAKUU WA SHULE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here