Na: Stella Kessy, DAR
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Ajibu Migomba amesaini mkataba wa mwaka mmoja Azam FC.
Ajibu alifanikiwa kuchezea Simba na baadae alienda Yanga na kurejea klabu yake ya zamani, Simba SC kutoka kwa mahasimu, Yanga SC.
Taarifa ya Azam Fc jana mchana imesema kwamba Ajibu amejiunga hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Hata hivyo Simba imetoka taarifa kuwa wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu baada ya kuangalia faida za pande zote.
Ajibu ni mchezaji kijana mwenye uwezo mkubwa Lakini hakupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwahiyo ili kulinda kipaji chake simba walimruhusu kwenda kutafuta timu itakayompa nafasi.
Kipaji cha ajibu kilionekana akiwa katika timu ya simba ya vijana Simba B kabla ya kupandishwa kwa wakubwa ambapo pia alionyeshwa uwezo mkubwa.
Hata hivyo klabu ya simba inamtakia kila kheri Ajibu katika maisha yake mapya ua soka nje ya Simba ni matumaini ataendelea kuonyesha uwezo kwa ana kipaji kikubwa