Home LOCAL HOSPITALI 13 ZA RUFAA ZA MIKOA ZAKABIDHIWA RAMANI ZA VYUMBA VYA KUSAFISHA...

HOSPITALI 13 ZA RUFAA ZA MIKOA ZAKABIDHIWA RAMANI ZA VYUMBA VYA KUSAFISHA DAMU




Dar es Salaam

Timu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Bohari ya Dawa (MSD) imewakabidhi wawakilishi wa Hospitali za Rufaa 13 za Mikoa nchini ramani zilizopendekezwa kwa ajili ya kukarabati na kujenga vituo vya kusafisha damu kwa wagonjwa wa Figo.

Hatua hii imekuja baada ya MSD kuwezesha upatikanaji   wa mashine na vitendanishi vya kusafisha damu kwa gharama nafuu.

Kwa mujibu wa Mfamasia  Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi huduma hizo zinatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao kwa hospitali zitakazokuwa zimekamilisha jengo na miundombinu.

Aidha, Bw. Msasi amewataka wakurugenzi wote wa hospitali hizo kutoa ushirikiano kwa MSD ili kuwezesha Serikali kupunguza gharama za Huduma ya kuchuja Damu nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here