Ghana na Liberia leo zinakutana katika fainali ya Michuano ya Soka Afrika kwa watu wenye Ulemavu (CANAF) inatarajia kufanyika kesho katika dimba la Benjamini Mkapa Dar Es Salaam.
Hata hivyo Ghana ilipata nafasi ya kufuzu fainali baada ya kuitandika mabao 3_1 dhidi ya Angola ,huku Liberia imepata nafasi hiyo baada ya kuichapa bao 1_0 dhidi ya Tanzania katika michezo ya hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo iliyofanyika juzi kwenye Uwanja huo.
Kwa matokeo hayo nafasi ya mshindi wa tatu Tanzania watamenyana dhidi ya Angola katika Mchezo utakaochezwa kesho kwenye uwanja huo.
Naye Rais wa Shirikisho la soka la wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi,amesema kuwa anamshukuru mungu kwa jambo la kujivunia licha ya kukosa matokeo mazuri na ni sehemu ya kujifunza.
Amesema kuwa Tanzania ilipata nafasi nyingi lakini ikishindwa kuzitumua kwa wakati, hivyo wapinzani wakatumia na kuibuka na ushindi .
“Wapinzani wetu wna uzoefu na wamechukua makombe matatu na tuangalie ,hivyo kwa muda uliobakia kocha ataweza kuyafanyia kazi mapungufu ikiwamo ya ushambuliqji na umaliziajikabla kuelekea kombe la Dunia,” amesema Sarungi.