Home LOCAL DCEA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA TAASISI ILIYOANDAA VIZURI TAARIFA ZA MAHESABU 2020

DCEA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA TAASISI ILIYOANDAA VIZURI TAARIFA ZA MAHESABU 2020


 
 

Mamalaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekuwa Mshindi wa kwanza na kupata tuzo mbili za taasisi iliyoandaa vizuri taarifa za mahesabu kwa mwaka 2020.

Tuzo ya kwanza ni katika Kundi la Wizara na Idara zinazojitegemea (MDAs) za Kiserikali iliyo andaa vizuri Hesabu kwa Viwango vya Kimataifa kwa Sekta ya Umma (IPSAS) kwa mwaka huo na ya pili ni ya Mshindi wa jumla kwa MDAs zinazotumia IPSAS.

Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo Gerald Musabila Kusaya wakati akipokea tuzo hizo, ameeleza kuwa, mbali na Mmlaka kuweka mkazo katika kutekeleza majukumu yake ya udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya bado imekuwa na umakini mkubwa katika kusimamia matumizi ya fedha.

Aidha, ameeleza kuwa, umakini huo ndiyo umeifanya Mamlaka kuendelea kupata ushindi huo mfululizo ambao ni wa nne sasa.
 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here