Home SPORTS CAMBIASO SPORTS ACADEMY YAMPELEKA KIJANA WAO OMARY MVUNGI KUJIFUNZA SOKA UK

CAMBIASO SPORTS ACADEMY YAMPELEKA KIJANA WAO OMARY MVUNGI KUJIFUNZA SOKA UK


NA: STELLA KESSY

KITUO Cha kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana, Cambiaso Sports Academy kimeendekeza kutimiza ndoto za vijana baada ya Kumpeleka kijana wao, Omary Mvungi Uingereza kwa ajili ya mafunzo ya mpira wa miguu.

Akizungumza Dar es Salaam leo na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Cambiaso, Twaha Ngwambi amesema kituo hicho kinampeleka  Omary  Mvungi kwenda nchini Uingereza kwa ajili ya kufanya mafunzo ya soka na kuendeleza kipaji chake cha mpira.

Ngwambi amesema kuwa mafunzo ni muda wa miezi sita  yatayofanyika katika kituo cha Garuda programu katika kambi ya mchezaji wa zamani wa Charles, Dennis Wise.

“Atakuwa Uingereza kwa muda wa miezi sita kwa ajili ya kufunza na kupata uzoefu wa soka,” amesema.

Amesema Omary anaandaliwa kwa ajili ya kuja kuwa mchezaji Bora na kucheza sok la kimataifa.

“Mchezaji huyu anaandaliwa ili aje kucheza soka la kimataifa kuonyesha uwezo wake, hivyo sasa anapikwa na kuwekwa fiti zaidi,” amesema.

Mchezaji  Omary Mvungi amesema kuwa nafuraha kuchaguliwa kwenda Uingereza kwani ni ndoto zake zilikuwa muda wote.

Pia  alitoa shukrani kwa uongozi wa Cambiaso na wazazi wake kumpa ushirikiano katika kutimiza ndoto zake.

“Maandalizi mazuri yanatokana na fursa naona ndoto yangu inakujaa kutimiza katika kucheza soka la kimataifa, “ amesema.

Omary aliwaomba mashabiki na wapenzi wa soka kumpa sapoti ili malengo yake yaweze kutimia.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here