Home BUSINESS BITEKO AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI ZAIDI YA 8 KWA UBADHILIFU

BITEKO AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI ZAIDI YA 8 KWA UBADHILIFU

Na: Saimon Mghendi, Kahama

WAZIRI wa madini Mhe,Dkt, Doto Biteko, ameamuru kusimamishwa kazi kwa Maafisa Madini Zaidi ya 8 kwa tuhuma za ubadhilifu wa mirahaba ya serikali jambo hadi pale uchunguzi utakapo kamilika na sheria kuchukua mkondo wake.

Waziri Biteko ameyasema hayo leo kwenye mkutano maalumu uliowakutanisha watumishi wa Wizara ya madini pamoja na wadau wa madini, Mkutano ambao umefanyika katika Manispaa ya Kahama nakuudhuriwa na wadau wa madini kutoka mikoa mbalimbali.

Aidha Waziri Biteko amesema kuwa watumishi hao wamekua wakipunguza kodi ya serikali wanayokusanya na kupeleka pungufu huku wengine wakitumia njia ya kushusha thamani ya dhahabu kwakutumia mashine maalimu zinazotumika kupima dhahabu kwa lengo la kujinufaisha.

“Waliokua wanatorosha madini ni wafanya biashara sasa wafanyabiashara wamerudi kwenye msingi na wamebaki wachache na ugonjwa huo umeamia kwa watu wetu wa madini na ndio kilichonileta hapa kwa sababu hapa kuna matatizo”,amesema Waziri Biteko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here