Home BUSINESS AVUMBUA MADINI YA DHAHABU WAKATI AKICHIMBA SHIMO LA CHOO

AVUMBUA MADINI YA DHAHABU WAKATI AKICHIMBA SHIMO LA CHOO

Na: Saimon Mghendi, Mbogwe, Desemba 10,2021.

MWANAKIJIJI mmoja wa Kijiji cha Kakumbi Kata ya Lugunga, Wilayani Mbogwe, Mkoani Geita, Said Tangawizi amegundua Madini ya Dhahabu wakati akichimba shimo la choo kwenye eneo lake la uwekezaji wa ghala la kuhifadhia mazao.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni kijijini hapo ambapo mara baada ya kugundulika madini hayo, Serikali ya Kijiji ilikaa kupitia mkutano halali na wakazi wa eneo hilo kwa lengo la kufanya maridhiano ili kubadili matumizi ya eneo husika kutoka kwenye makazi kuwa eneo la uchimbaji.

Baada ya mkutano wa serikali ya Kijiji hicho cha lugunga, Tangawizi  alisema kuwa neema hiyo imetokea juzi wakati vibarua aliowatuma kuchimba shimo la choo kwenye ghala lake linalotumika kuhifadhia mazao ya nafaka, wachimbaji hao walikutana na mwamba unaosadikiwa kuwa na madini ya dhahabu na alipoyachukua kwalengo la kuyapima kiasili(Kupiga chabo) mawe hayo yalionekana kuwa na Dhahabu nyingi.

“Baada ya kupatikana Madini ya dhahabu kwenye shimo la choo kwakweli nilichukua hatua ya kuieleza serikali ya Kijiji kupitia Afisa Mtendaji wa Kata na baadaye Diwani ambaye alipeleka taarifa hizi ofisi ya Madini ili kupata utaratibu maalumu,” alisema Tangawizi.

Vile vile Tangawizi alisema kuwa licha ya wananchi kukubaliana kuchimba dhahabu kwenye eneo hilo yeye binafsi alilidhia eneo lake lichimbwe Dhahabu huku akitambua kuwa sheria ya madidini inamtaka wazi kuwa madini ni mali ya serikali hata yangetokea maeneo tata.

Diwani wa Kata ya Lugunga Enock Magulu akizungumzia hali hiyo alisema kuwa alipata taarifa hizo kupitia afisa Mtendaji wa Kata na alipofuatilia Zaidi ofisi za Madini waliomtaka athibitishe madai hayo alifika kwenye eneo hilo na kuruhusu kuchimbwa kwa maduara manne na kujiridhisha kuwa kuna madini ya Dhahabu.

“Kiukweli baada ya hapo serikali ya Kijiji iliitisha mkutano wa hadhara wa waanchi ili kupata maoni yao na kupitia mkutano huo wananchi walilidhia eneo la Kijiji chao kichimbwe Madini hayo ili wapate maendeleo,” alisema Tangawizi.

Hata hivyo wakitoa maoni yao juu ya mlipuko huo wa Madini ya dhahabu  wananchi wa Kijiji hicho Pendo John Pamoja Ntemi Mtoka wameiomba serikiali kuruhusu eneo hilo lichimbwe kwa kuwa wao wenyewe wameridhia kupitia mkutano wa hadhara eneo hilo lichimbwe kusitokee pingamizi lolote.

“Tuwakumbushe tu viongozi kuwa sisi tupo tayari kutumia fursa ya raslimali hii iliyopatikana kijijini kwetu kwamba tuitumie kupata maendeleo yet una Kijiji kwa ujumla lakini kutokana na mlipuko huu kuibukia kwenye makazi ya watu wakumbuke suala la kuhifadhi mazingira maana ummati wa watu utakuwa mkubwa,” alisema Ntemi Mtoka mkazi wa Kijiji cha Kakumbi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kakumbi, Jonathan Mahega alithibisha kutokea kwa mlipuko wa madini hayo na kusema kuwa Wananchi walirdhia kubadilishwa matumizi ya eneo hilo kutoka makazi kuwa eneo la uchimbaji kupitia mkutano halali wa Kijiji.

“Kwa kweli kama kiongozi wanakijiji walinifurahisha sana na wanapenda maendeleo, hii neema iliyoletwa na Mungu wananchi tumekubaliana tuchimbe dhahabu ili tupate maendeleo na hakuna mgogoro wowote,” alifafanua Mahega mwenyekiti wa kitongoji cha Kakumbi Mbogwe.

Mwisho.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here