Home SPORTS YANGA YAIPA KICHAPO MBEYA KWANZA 2-0

YANGA YAIPA KICHAPO MBEYA KWANZA 2-0

 

Na: Mwandishi wetu, MBEYA.

MABINGWA wa kihistoria  Yanga SC leo wameichapa Mbeya kwanza ametanua  jioni ya leo katika michuano ya ligi  kuu ya Tanzania bara katika mchezo uliopigwa katika  Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 18 na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 26 akimalizia pasi ya kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’.

Kwasasa Yanga SC inafikisha pointi 19 baada ya mechi saba huku wapinzania wao Mbeya Kwanza wanabaki na pointi zao saba za mechi saba katika nafasi ya 11.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here