Home SPORTS YANGA WATUA ZENJI KUJIFUA

YANGA WATUA ZENJI KUJIFUA

Mwandishi wetu..

KIKOSI  cha Yanga leo umewasili Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na kujiimarisha zaidi kuelekea michezo yao ya NBC Premier league.

Msafara huo wenye wachezaji 22 benchi la ufundi lenye watu 10 na viongozi 4 utakaa  hapa Zanzibar kwa takriban siku nne ambapo mashabiki wa klabu hiyo wataishuhudia timu yao ikicheza mechi mbili za kirafiki.

Akizungumza Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wameona vizuri kuja Zanzibar kutokana na historia ya klabu hiyo, ambapo Leo Novemba tisa saa 2:00 usiku kwenye dimba la Amaan  watacheza mechi ya kirafiki na timu ya Mlandege inayoshiriki ligi kuu Zanzibar na Ijumaa watacheza na bingwa mtetezi KMKM.

Kwa upande wa afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema ziara hiyo maalum kwa ajili ya mechi za kirafiki kwa sababu kocha wao alitaka mechi mbili za kirafiki kwaiyo baada ya kupata  mualik kutoka Serekali ya Zanzibar hivyo wameona mechi hizo za kirafiki kuzicheza wakiwa hapa .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here