Home BUSINESS WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA...

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAANDAA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA UINGEREZA



DAR ES SALAAM.

Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Ubalozi wa Uingereza hapa nchini pamoja na Taasisi ya Sekta Bianafsi Tanzania (TPSF) imeratibu maandalizi ya kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Uingereza (Tanzania – UK Business Forum) litakalofanyika tarehe 16 Novemba 2021 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha JNICC Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa Kongamano hilo litafunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), na kuhidhuriwa pia na Mjumbe Maalum wa masuala ya Biashara wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Lord John Walney na kwamba washiriki takriban  200 kutoka Serikali na Sekta Binafsi za nchi zetu mbili watahudhuria Kongamano hilo na wengine wengi zaidi watashiri kwa njia ya mtandao.

“Kongamano hilo limeandaliwa kwa namna ya kipekee ili kuongeza tija ya matokeo tarajiwa ambapo limegawanyika katika makundi makundi matatu yatakayofanya mijadala kwa wakati mmoja” ameeleza Prof. Kitila.

Aidha pamoja na mambo mengine Kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki ujadiliana kwa kina na kubaini fursa mpya za Ushirikiano ya nchi hizo mbili, ambapo pande hizo mbili zitaweza kutanua wigo wa ushirikiano katika maeneo ya Biashara na uwekezaji hususan katika Sekta za Nishati, Madini, Miundombinu, Kilimo, uchumi wa buluu na utalii.

“Nchi za Tanzania na Uingereza zina Mahusiano ya karibu ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakiimarika siku hadi siku kutokana na mashauriano ya mara kwa mara baina ya Serikali za pande zote mbili” Ameongeza Waziri Mkumbo.

Kwa mujibu wa takwimu za kituo cha uwekezaji (TIC), nchi ya uingereza ni ya pili kwa uwekezaji hapa nchini ikiwa na miradi takriban 945 yenye thamani ya Dola za Marekani 5.42 Bilioni na utoa ajira takriban 275,384. Aidha kwa Mujibu wa Serikali ya Uingereza, jumla ya thamani ya Biashara baina ya nchi hizi mbili kwa mwaka 2021 ilikuwa Pauni za Uingereza 156 milioni huku uingereza ikiuza hapa nchini Bidhaa zenye thamani ya Pauni 127 milioni na tanzania ikiuza Uingereza Bidhaa zenye thamani ya Pauni 29 Milioni. 

Pamoja na mambo mengine Kongamano hilo linalenga kujadili na kuridhia mikakati ya pamoja itakayolenga kupunguza pengo la Biashara kwa kukuza zaidi mauzo ya Bidhaa za Tanzania nchini Uingereza ambapo kauli mbiu ya Kongamano hilo ni “Kuimarisha Ustawi Endelevu wa Kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here