Home LOCAL WAZIRI UMMY MWALIMU AWAPONGEZA VIONGOZI HALMASHAURI YA TEMEKE

WAZIRI UMMY MWALIMU AWAPONGEZA VIONGOZI HALMASHAURI YA TEMEKE



Na: Mwandishi Wetu.

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewapongeza viongozi wa Temeke, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Mkurugenzi pamoja na watumishi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 15,2021 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na benki ya Dunia, kupitia miradi ya kimkakati ya uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam (DMDP).

Miradi hiyo ambayo ilikua kwenye awamu ya kwanza ya utekelezwaji wake, kwa sasa imekamilika na imekua chachu kubwa ya maendeleo na faida kwa Wananchi,huku zaidi ya bilioni 650 zikiwa zimetumika  katika utekelezwaji wake  kwa manispaa ya Temeke.

Waziri Ummy alitabanaisha kwamba kupitia fedha za benki ya Dunia, katika kuboresha huduma za jamii ,miundombinu ya Dar es Salaam ikiwemo kujenga barabara,vituo vya afya na masoko,maeneo mengi katika jiji yamebadilika na kupendeza.

Aidha amewashukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano huo,mbali na shukrani hizo, amewaomba kwamba katika  awamu zijazo,waongeza ushirikiano katika kuboresha maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa na mradi huo.

Katika ziara hiyo Ummy amewangozana na viongozi mbalimbali wa benki ya Dunia akiwemo Mari Pangestu ambaye ni mkurugenzi wa sera, maendeleo na ushirikiano wa benki hiyo. Kwa pamoja walitembelea soko la Makangarawe na kituo cha afya Buza.

“Sekta ya afya imeimarika, vituo vipo vizuri, visafi, lakini tangu kituo hicho kimeanza kutoa huduma, hawajapata kifo kinachotokana na ujauzito au uzazi, kwa hilo amewapongeza sana,”amesema Waziri Ummy.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here