Home LOCAL WAZIRI MCHENGERWA: WALIOGUSHI VYETI HAWAJARUDISHWA KAZINI BALI WALE WALIONDOLEWA KWENYE ORODHA...

WAZIRI MCHENGERWA: WALIOGUSHI VYETI HAWAJARUDISHWA KAZINI BALI WALE WALIONDOLEWA KWENYE ORODHA KIMAKOSA.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa imma na utawala bora Mohamed Mchengerwa  ametoa ufafanuzi juu ya uvumi unaendelea nchini kuwa watumishi waliondolewa kutokana na kuwa na vyeti feki wamerudishwa kazini jambo ambalo amesema sio kweli kwani waliorudishwa na kulipwa mishahara ni  watumishi 4,380 waliondolewa kimakosa wakati wa zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi hewa.

Waziri Mchengerwa aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha ambapo alisema kuwa idadi hiyo inajumuisha watendaji wa kata, vijiji na mitaa wapatao 3,114 ambapo pia serikali imetoa msamaha wa kuwarejesha kazini watumishi waliondolewa kazini kwa kukosa sifa ya Elimu ya kidato cha nne na baadaye kujiendeleza na kupata sifa tajwa Hadi kufikia Disemba 2020 ambao hawakudanganya katika taarifa zao kuwa wana elimu ya kidato cha nne au kubainika kughushi vyeti.

Alisema kuwa msamaha iliyotolewa unawahusu watumishi walioajiriwa baada ya tarehe 20 Mei 2004 bila sifa ya Elimu ya kidato cha nne na baade kujipatia sifa za kuajiriwa na hauwahusu watumishi waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi au waliotoa taarifa za uongo katika kumbukumbu zao rasmi za utumishi.

“Serikali imelipa madai ya mishahara zaidi ya bilioni 2 na million 613 kwa watumishi 1,643 waliorejeshwa kazini baada ya kuondolewa kwenye orodha ya malipo kimakosa na uhakiki wa madai yaliyobaki yanaendelea na yataendelea kulipwa kwa kadri uanavyohakikiwa, Alisema Mchengerwa.

Aidha alitoa taarifa kuhusu maadhimisho ya miaka ya miaka 60 ya Uhuru ambapo alisema kuwa kwa kipindi chote cha miaka 60 ya Uhuru utumishi wa umma imeendelea kuwa uliotukuka katika kuchangia ustawi wa taifa ambapo ofisi hiyo ina hukumu la kusimamia utekelezaji wa sera, Sheria na kanuni za utawala wa utumishi wa umma na usimamizi wa rasilimaliwatu  na taratibu za uendeshaji wa utumishi wa umma.

Alisema kuwa serikali katika miaka yote 60 ya Uhuru kumekuwa na ongezeko la ajira katika utumishi wa umma kutoka watumishi 17,565 mwaka 1961 Hadi kufikia 528,290 mwezi October ambapo Kati yao watumishi wa sekta ya afya Ni 72,961 sawa na asilimia 13.8 na walimu 281,729 sawa na asilimia 53.3.

Alisema pia wakifanikiwa kuwaondoa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi 15,578 waliobainika kughushi vyeti vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne, cha sita na ualimua kati ya watumishi 535,770 waliohakikiwa ikiwa ni pamoja na kuwaondoa  katika malipo ya mishahara watumishi 5,335 walioajiriwa katika utumishi wa umma kinyume na sifa ya maendeleo ya kiutumishi.

“Lakini pia tumefanikiwa kuwaondoa katika orodha ya malipo ya mishahara watumishi hewa 19,708 na kuiwezesha serikali kuokoa jumla ya  shilingi bilioni 19.84 pamoja na mambo  mengi  ambayo tumefanikiwa,” Alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here