Na: Heri Shaaban.
JUMUIYA ya Wazazi Wilaya imeanza mikakati ya kujenga nyumba ya Katibu wa Wazazi wa Wilaya Ilala.
Mkakati huo umenza hivi karibuni kufuatia Mtumishi wake kukosa nyumba kuishi.
Akizungumza katika Bonanza la Wazazi Dar Salam Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala , Mohamed Msophe
alisema mkakati huo wa kujenga umeanza hivi karibuni kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo na wenye mapenzi mema na chama.
“Chama ni chetu ,Jumuiya hii ni yetu tunawaomba wadau wa maendeleo ,na wenye mapenzi mema ya chama eneo letu lipo Buyuni la Jumuiya yetu ya Wazazi ndio tutajenga nyumba ya mtumishi wetu Katibu wa Wilaya taratibu zote zimeanza hivi karibuni tutazindua rasmi nawaomba tushirikiane kwa pamoja kusaidia Chama na Jumuiya yetu ” alisema Msophe .
Msophe aliwaomba wadau waliokuwa tayari kuchangia wawasilishe Wilayani ofisi za Jumuiya ya Wazazi watapewa taratibu zote namba ya kulipia akaunti ya Jumuiya ya Wazazi Contro namba.
Akizungumzia Bonanza la Michezo alisema dhumuni lake kuwaita wanachama wote wa Jumuiya ya Wazazi kuwasajili katika utaratibu unaotambulika waweze kuwatambua kwa ajili ya kuunda vikundi kila kata kwa ajili ya kuwainua kiuchumi waweze kupata mikopo ya Serikali wajiwezeshe kiuchumi .
“Siasa na Uchumi kila kata Jumuiya yetu inatakiwa wabuni miradi ya maendeleo itakayowawezesha jumuiya yetu kusimama imara “ alisema .
Shamsudini alisema katika bonanza hilo wametoa zawadi mbalimbali kwa mabingwa ikiwemo ,Mbuzi ,jezi na mipira kwa ajili kwa Washindi.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu MNEC Wazazi Taifa Selemani Juma Kimea alipongeza Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala kwa kubuni jambo kubwa kuweka Jumuiya Pamoja kwa ajili ya kujenga Chama na jumuiya zake
MNEC Selemani Juma Kimea alisema michezo ina jenga Afya udugu na Mshikamano hivyo aliwataka Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala pamoja na Wanachama wake kujenga umoja na mshikamano kwa ajili ya kujenga chama na kukitangaza chama.
Mwisho