Home LOCAL WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA WATOA SHUHUDA ZAO MBELE YA DCEA NA...

WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA WATOA SHUHUDA ZAO MBELE YA DCEA NA JOPO LA WAANDISHI WA HABARI, MOROGORO #KataaDawazaKulevya_TimizaMalengoyako


 

MOROGORO.

Waraibu wa Dawa za Kulevya waliopo kwenye kituo cha upataji nafuu cha Free at Last Mjini Morogoro wameeleza sababu zilizowapelekea kujihusisha na matumizi ya Dawa hizo mbele ya waandishi wa habari na Maofisa kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) walipowatembelea kwenye kituo chao.

Waandishi hao walifika Kituani hapo ikiwa ni siku ya pili ya Kikao Kazi cha siku tatu kwa waandishi wa habari za Kidigitali kilichoandaliwa na DCEA Mjini Morogoro kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao kufahamu mikakati ya Mamlaka hiyo katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya ili kuweza kuifikia jamii na umuhimu wa wao katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu na ufahamu wa kutosha juu ya masuala ya Dawa za Kulevya na namna wnavyoweza kujihepusha na matumizi ya Dawa hizo.

Akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi Mkurugenzi wa Kituo hicho Michael Kassian ameishukuru DCEA kwa kuwaongoza waandishi wa habari kuwatembelea kwenye kituo chao nakwamba hiyo imekuwa fursa kwao kuweza kueleza changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kwa kuamini jamii itafikiwa na taarifa zinazohusu changamoto zitokanazo na matumizi ya Dawa za Kulevya.

“Tunashukuru kwa ushirikiano tunaupata kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, wamekuwa wakitoa kila aina ya ushirikiano kwetu.Tunafaraha kuwaona waandishi wa habari ambao wamefikiria kuja kwetu na tunaamini kama tutashirikiana na vyombo vya habari tutafika mbali,”amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Florance Khambi amewaeleza waandishi wa habari sababu za kutembelea kituo hicho na kusema kuwa Tume imeonelea ni vema waandishi wa habari kufika kituoni hapo ili kujifunza namna ambavyo waraibu hao wanavyoishi na kupata matibabu ili kuihabarisha jamii juu ya tatizo la Dawa za kulevya nakwamba tatizo hilo linatibika.

“Tumekuja hapa tukiwa kwenye ziara ya mafunzo , tuko na wanahabari za kidigitali, kwa hiyo tumefika hapa kwenye nyumba ya utengamao ya Sobae House Free at last kujifunza”.Ameongeza Florence.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here