Home BUSINESS WANAWAKE WAASWA KUAMKA KUUSAKA UTAJIRI

WANAWAKE WAASWA KUAMKA KUUSAKA UTAJIRI

Na: Oscar Job

WAJASIRIAMALI wanawake nchini wameaswa kutumia mbinu mbalimbali za kibiashara ili waweze kujiinua na kuwa wafanyabiashara wakubwa jambo litakalowafanya waweze kupiga hatua zaidi za kimaendeleo.

Rai hiyo imetolewa jana na Afisa Biashara wa Mkoa wa Dar es Salaam Thabit Massa wakati wa uzinduzi wa jumuiya ya wanawake wajasiriliamali ‘Woman Rich Forever’ ambavyo lengo lake ni kuwahamasisha wanawake kujiinua kibiashara.

Alisema ilo kufikia lengo hilo wanawake hao wanapaswa kuachana na fikra za kwa  kujiita wafanyabiashara wadogo kila siku na badala yake watumie fursa zilizopo nchini kutimiza malengo yao ya kila siku.

“Naamini kama mtatumia vizuri fursa ya jumuiya yenu mtaweza kufika mbali na hivyo kujiletea maendeleo yenu binafsi na Tanzania kwa ujumla, mkifanya hivyo mtaweza kujiinua nyie wenyewe binafsi na Taifa kwa ujumla” alisema 

Kwa upande wake muasisi wa Jumuiya hiyo ya ‘Rich Woman Forever’ Amina Ntomola alisema wamejiita ‘Rich Woman Forever’ kama chachu kwa mwanamke yeyote mwenye ndoto za kutimiza malengo mbalimbali ya kimafanikio.

Alisema kupitia tukio la Rich Woman Event, wamelenga kuwapa elimu wanawake wote na mbinu za kufanikiwa katika biashara, afya na mahusiano wakiamini kwa kufanya hivyo kutamuwezesha  mwanamke kufanikiwa.

Alisema kwa kuanza tukio hilo limeanza kwa kuwahusisha wanawake wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na zaidi limelenga kumfanya mwanamke kuwa shujaa katika dhamira yake.

“kupitia umoja huu pia tunataka kuisadia jamii katika nyanja mbalimbali ili waweze kuondokana na changamoto mbalimbali za kimaisha na hivyo kusaidia kutimiza ndoto zao” Amina.

Alisema kuanzishwa kwa umoja huo ni fursa kwa jamii hususani ya wanawake kufanikiwa kimaisha na hivyo kutimiza malengo yao ya kimaisha sambamba na kuwezesha maendeleo ya Taifa kwa ujumla

Aidha walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa anazozifanya kuliletea Taifa maendeleo sambamba na kurejesha mahusiano ya kimataifa hivyo kuongeza chachu ya uwekezaji nchini.

Kwa upande wake mdhamini wa tukio hilo ambaye no Mkurugenzi wa ‘Magari Mazuri Tanzania’ Stephan Mapunda alisema kwake wanawake ni watu wa thamani kutokana na hatua kubwa wanazoendelea kuzipiga katika kujiletea maendeleo.

Alisema wanachopaswa kufanya wanawake hao ni kuhakikisha wakati wote wanatumia fursa wanazozipata kujiletea maendeleo.

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here