Home LOCAL WANANCHI RUANGWA WAPONGEZA MASHIRIKA YA KUHIFADHI MISITU KWA KUTATUA MGOGORO SUGU WA...

WANANCHI RUANGWA WAPONGEZA MASHIRIKA YA KUHIFADHI MISITU KWA KUTATUA MGOGORO SUGU WA ARDHI



Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya



Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu wilayani humo mkoani Lindi katika mkutano uliofanyika jana

Afisa Ufuatiliaji na Utafiti wa Shirika la TFCG, Edward Emil akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma.


Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge.




Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Nolasco Kitumile akizungumza na waandishi wa habari.

Wajumbe wa kamati mbalimbali wa Kijiji cha Malolo wakiserebuka kabla ya kuanza mkutano huo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Malolo Wilbert Mwambe akizungumza kwenye mkutano uliofanyika kwenye kijiji hicho wakati wakitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa waandishi wa habari..

Afisa Misitu wa Wilaya ya Ruangwa James Kabuta akizungumza kwenye mkutano huo.

Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge akizungumza kwenye mkutano huo.

Diwani wa Viti Maalumu wa Kata hiyo Ansila Lukanga akichangia jambo kwenye mkutano huo.


Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Mwalimu Mohamed Abdallah akiendesha kikao hicho.

Mkazi wa kijiji hicho Gerald Mwambe akizungumza kwenye kikao hichoMzee Maarufu wa kijiji hicho Mohamed Abdallah akichangia jambo kuhusu utunzaji wa misitu.

Mkutano ukiendelea.

Mjumbe wa Kamati ya Maliasili Hilda Mwambe akichangia jambo kwenye mkutano huo.


Mkutano ukiendelea.


Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Malolo, Abdallah Said akizungumza kwenye mkutano huo.


Picha ya pamoja.

 Na: John Bukuku. Ruangwa Lindi.

WANANCHI wa Kata ya Malolo wilayani Ruangwa mkoani Lindi wameyapongeza Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA) yanayo fadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC) kwa kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi uliyohusisha Kijiji cha Malolo na Kijiji jirani cha Ng’au.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mbele ya waandishi wa habari ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu wilayani Ruangwa mkoani hapa walisema mashirika hayo yalifanikiwa kuumaliza mgogoro huo kwa amani na utulivu.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Wilbert  Mwambe alisema kumalizika kwa mgogoro huo kumesaidia kufungua fursa za matumizi bora ya ardhi na shughuli za uzalishaji endelevu wa mazao ya misitu kama, mbao, mkaa na kilimo.
“Hivi sasa hatuna ugomvi na wananchi wenzetu wa kijiji hicho ambao tulikuwa tukigombea eneo la ekta zaidi ya 2000 ambapo tulirudishiwa” alisema Mwambe.
Diwani wa Viti Maalumu wa Kata hiyo Ansila Lukanga aliyashukuru mashirika hayo kwa kutoa elimu kwa Wananchi wa Kijiji hicho ambao sasa wameanza kujua thamani ya misitu.
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Mwalimu Mohamed Abdallah alisema hivi sasa wananchi wa eneo hilo wanahamasa kubwa ya kuinuka kiuchumi baada ya kujua thamani na matumizi bora ya ardhi na tayari wamekwisha tenga maeneo ya makazi, kilimo na ufugaji baada ya kupatiwa elimu hiyo.

Wazalishaji wa mbao na mkaa katika kijiji hicho wameyaomba mashirika hayo kuwatafutia masoko ya bidhaa hizo ambayo hayapo licha ya kuwa na mkaa magunia 40 ambayo wameyavuna kutoka katika misitu msitu wao kwa kufuata sheria.

Wananchi hao wamesema kabla ya kupelekewa mradi huo na mashirika hayo hatukuwa na matumizi bora ya ardhi kwani walikuwa wakikata miti kiholela jambo lililokuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuhalibu mazingira na misitu.

Awali akizungumza na waaandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma alisema misitu ni lazima ilindwe na akatumia nafasi hiyo kuyashukuru mashirika hayo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuisaidia Serikali kutunza misitu ya asili katika wilaya hiyo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Nolasco Kitumile alisema halmashauri hiyo imetenga sh.12 milioni kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa misitu katika vijiji viwili vya Nangulugai na Nalung’ombe na kuwa Halmashauri hiyo ina misitu sita iliyosajiliwa huku miwili ikifanyiwa mchakato wa kusajiliwa ambapo itakuwa na misitu 8 ukiwepo na wa halmashauri.

Mashirika hayo yanatekeleza mradi huo katika wilaya ya Kilosa, Mvomero, Morogoro, Liwale, Nachingwea na Ruangwa katika Kata ya Malolo. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here