Home LOCAL WANAKIJIJI WALALAMIKIA UONGOZI WA KATA KUHAMISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA RUFIJI

WANAKIJIJI WALALAMIKIA UONGOZI WA KATA KUHAMISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA RUFIJI

Na: Mwandishi wetu Rufiji.

WANANCHI wa kijiji cha Ngorongo kata ya Ngorongo  Wilayani Rufiji Mkoani pwani  wameulalamikia uongozi wa kata hiyo chini ya Diwani Hassan Mpange kuhamisha ujenzi wa kituo cha Afya  kilichokuwa kijengwe kijijini hapo.

Wamesema viongozi hao wamefanya maamuzi hayo kwa matakwa yao na si kwa makubaliano na wananchi na kwamba ujenzi huo wanaupeleka  Kilimani hali ambayo inawachanganya wananchi wa kata hiyo.

Wakizungumza kijijini hapo mbele ya waandishi wa habari kupitia mkutano wa dharula ulioitishwa na wananchi hao.  wamesema  awali walikubaliana kituo hicho kijengwe katika kijiji cha Ngorongo na tayari kilikuwa kimeshaanza kujengwa  kwa nguvu za wananchi na Serikali akiwemo Mbunge wa jimbo hilo Mohamed Mchengerwa ambaye alichangia Fedha na mifuko ya Saruji  . 

Mwenyekiti wa kijiji hicho Rajabu Ally akizungumzia sakata hilo amesema Baada ya kuingizwa pesa za ujenzi wa kituo hicho Diwani amekuwa na kauli zisizo waridhisha wananchi wake na kuamua kuachana na  Kituo cha awali na kuanza mchakato wa kufyeka msitu mwingine ili kijengwe kituo cha Afya kingine kinyume na makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa. 

“Jambo hili limechanganya wananchi na ndio maana umeona mkutano huu wa dharula .wananchi hawakubaliani na hiki kunachofanyika na viongozi ngazi ya kata.”amesema Mwenyekiti Ally

Kwaupande wake Sud Mohamed amesema ili kupata ufumbuzi wa jambo hilo wanamuomba rais Samia Hassan Suluhu amemuomba  Kuitupia Macho kata ya Ngorongo  haswa Diwani wao ambae wamedai kuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya kata Yao.

Ameongeza kuwa hawakubaliani na hatua ambayo diwani aneichukua ya kuhamisha ujenzi wa kituo hicho cha afya nakwamba wananchi wametumia nguvu nyingi kuhakikisha eneo hilo linajengwa Zahanati. 

Naye Diwani Mpange anayelalamikiwa akizungumzia malalamiko hayo ya wananchi wa kijiji cha Ngorongo amesema yeye kama diwani hana uwezo wa kubatilisha au kuhamisha ujenzi wa kituo hicho lakini hatua hiyo imefikiwa kupitia bazara la ODC ambalo linashirikisha wenyeviti wote wa serikali za mitaa. 

Amesema Kuwa walikubaliana kwa pamoja tena baada ya kujiridhisha kwamba eneo ambalo linakwenda kujengwa kituo cha afya ni rafiki na limezingatia uwiano wa vijiji vyote vinne vilivyopo ndani ya kata ya Ngorongo. 

“Ndugu mwandishi nimekupa ushirikiano wote juu ya uwepo wa malalamiko hayo lakini kama nilivyosema haya nimakubaliano kupitia baraza la ODC lakini pia watalaamu kutoka wilayani nao walishauri “amesema Mpange.

Pia ameongeza Kuwa kuhusu Zahati inayojengwa kwenye kijiji cha Ngorongo licha zahanati hiyo kujengwa kwenye eneo si rafiki yeye kama diwani kwa kushirikiana na Mbunge wao mchengerwa wamehaidi kutoa mifuko ya saruji 100 nahuku akishauri Zahanati hiyo isogezwe kwenye eneo lafiki kwasababu ilipo sasa panajaa maji.

Mwisho.
Previous articleWANAFUNZI UHASIBU WATAKIWA KUZINGATIA MASOMO HUKU WAKIANGALIA MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA
Next articleDCEA KUANDAA MWONGOZO WA ELIMU KWA JAMII KUHUSU MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here