Home LOCAL WANAFUNZI UHASIBU WATAKIWA KUZINGATIA MASOMO HUKU WAKIANGALIA MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA

WANAFUNZI UHASIBU WATAKIWA KUZINGATIA MASOMO HUKU WAKIANGALIA MAHITAJI YA SOKO LA AJIRA

Mwenyekiti wa bodi ya wahasibu wanawake Tanzania(TAWCA) Dkt.Neema Kiure akiongea na wanafunzi wa chuo cha uhasibu (IAA) katika maadhimisho ya siku ya uhasibu.

Mkuu wa chuo cha uhasibu (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka akiongea katika maadhimisho ya siku ya uhasibu yaliyofanyika katika chuo hicho mkoani Arusha.
 
Baadhi ya wanafunzi wanaochukua fakati ya uhasibu katika chuo cha uhasibu Arusha wakisikiliza jambo katika maadhimisho ya siku ya uhasibu.
NA: NAMNYAK KIVUYO ARUSHA.

Mwenyekiti wa bodi ya wahasibu wanawake Tanzania(TAWCA) Dkt.Neema Kiure amewataka wanafunzi wa vyuo wanaochukua fakati ya uhasibu kuzingatia kusoma kwa kuangalia  mahitaji ya soko la ajira ili kuweza kuisaidia serikali katika utambuzi wa mapato na manunuzi kwa njia ya kidijitali.

Akizungumza katika maadhimisho ya uhasibu duniani yaliyoadhimisha katika chuo cha uhasibu Arusha,Mwenyekiti wa  TAWCA,Dkt.Kiure alisema ni vyema wanafunzi wa fakati hiyo wakasoma kwa kuzingatia soko la ajira kutokana na mabadiliko ya teknolojia mbalimbali  kuwa za kiditali.

 Sambamba na hilo alisema katika fakati ya uhasibu wanawake wengi hupata vikwazo vya kutokuendelea mbele katika kufikia viwango vya juu vya elimu yao ya uhasibu yaani CPA hivyo kuna haja ya kuendelea kuwahamasisha ili kuendelea kupata uzoefu na ujuzi utakaowasaidia kubeba fursa zao kwani wanaweza jikuta shahada haitoshi.

“Ukipita kwenye vyuo wahasibu wa kike ni wengi lakini takwimu za watu wenye CPA zinaonyesha waliopo ni 2000 kwa asilimia 20 ndio walikuwa wanawake hivyo kuwepo kwa vikwazo vya kutokuendelea mbele ndio chanzo cha kushindwa kuweza kumaliza mitihani ya CPA,”alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema lakini kupitia TAWCA wanawake wengi wameonyesha nia yakufikia elimu ya juu yaani CPA hivyo wataendelea kuwahamasisha ili kuweza kufikia lengo la kukabiliana na changamoto zinazowakabili wahasibu na kuzipatia ufumbuzi.

Dkt.Kaure alisema sasa hivi wanazungumzia mapinduzi ya viwanda ndio changamoto kubwa zinazooneka kwenye ukaguzi wa mahesabu na uhasibu ukienda kwenye kampuni nyingi za uhasibu zinatumia uzoefu wa ujuzi wa IT hivyo kuna umuhimu wake wa kufahamu nyanja zote katika maisha ya Muhasibu.

Pia alisema mitaala ya elimu ya uhasibu haijitoshelezi kwani ukiangalia ukaguzi wa mahesabu aliyokuwa anafanya miaka 20 nyuma ni tofauti na sasa kwani hapo awali walikuwa wanatumia njia za kawaida za ukaguzi za kukaa na makaratasi na kukagua taarifa za mteja lakini sasa imekuwa tofauti sana.

“Sisi wahasibu na wakaguzi ndio walinzi wa nchi yetu kutokana na kazi ya kukagua mapato na matumizi na kama taarifa zetu hazieleweki zitakuwa hazina taswira nzuri kwa jamii pamoja na kampuni husika au taasisi,”alisema.

Hata hivyo alisema ni vyema wakazingati masomo wanayofundishwa ili yaweze kuwabeba katika sehemu za kazi kwa kujiamini na kuweza kukubalika kwenye soko la ajira.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha(IAA) Prof.Eliaman Sedoyeka alisema malengo yao ni kukifikia kuwa chuo bora Afrika cha uhasibu hadi kufikia 2025 kiwe bora nchini Tanzania hivyo wataendelea kukuza hifadhi kutokana na umuhimu wake.

“Ikiwa Muhasibu atayumba pia taasisi itayumba hivyo wakisimama vizuri pia taasisi itasimama vizuri kwani mitaala ya uhasibu imepanuka na kuhakikisha kwamba inacover maeneo yote ambayo itamwezesha mwanafunzi kuhakikisha anatoka hapa akiwa na ujuzi na weledi wa kukuwezesha wewe kufanya kazi yako,”alisema Prof.Sedoyeka.

Naye Makamo wa rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo,Avitha Mutayoba alisema wahasibu wanatoa michango mingi kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha rasilimali fedha na mikakati ya kifedha katika taasisi mbalimbali zinastawi katika miongozo na ustawi wa ukubwa  wa kibiashara.

“Pamoja na umuhimu huu wahasibu tumekuwa na changamoto ya uhitaji wa uzoefu kazini hasa katika ajira kututaka tuwe na uzoefu wa miaka mitatu,”Mutayoba alisema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here